Ijumaa, 23 Agosti 2019

TABIA ZA KUKWEPA ILI UFANIKIWE KIJASIRIAMALI NA KIMAISHA

Usikae bila shughuli yeyote
Epuka uvivu, Buni Kitu kitakachokupa fedha yaani shughuli ambayo ita kukeep busy, kwa kiwango kidogo

Usidharau ulivyo navyo
Haijalishi ni kidogo kiasi gani focus katika maono chanya kipende,kiheshimu, ongeza ubunifu na ukikuze,

Acha visingizio
Mafanikio ya mtu humtegemea yeye kwa 90%, Mafanikio yako yapo ndani yako, Usimlaumu au kumsingizia mtu.

Usiahidi uongo na usidhulumu MTU
  Ukitoa ahadi hakikisha unatekeleza na pia tenda haki, hapa tunazungumzia "Mahusiano" Jenga mahusiano mazuri na jamii inayokuzunguka kwani jamii yako ndiyo maendeleo yako

Usiwe tegemezi wa mawazo
Usiishi kwa mazoea,kufuata mkumbo au kufuata wanachotaka wengine, "Fanya unacho amini kuwa ni sawa"

Usikate tamaa
Unapokutana na magumu pambana nayo, unapo anguka simama, unapokosea jifunze, songa mbele na kamwe usiwe na woga,

Nikutakie utekelezaji mwema,
Mwl Massawe,

Ijumaa, 9 Agosti 2019

KABLA HUJARIPOTI CHUO SOMA HII

     Mkumbushe ndugu au rafiki yako kuwa maisha ya CHUO ni sawa na BONGO MOVIE watu wengi huigiza. Hata yule wa MBEYA vijijin atasema kwao MWANZA....

1. Mwambie anaenda kusomea taaluma sio kazi. Anaweza kusoma uhasibu akawa dobi...Anaweza somea Ualimu akawa mhudumu wa Bar au boda boda

2. Mwambie Kufaulu Taaluma sio Kufaulu maisha.wapo watu wenye elimu kumzid yeye ila hawana ajira. Hata wenye ajira bado maisha magumu

3. Mwambie Kupata alama nyingi sio kujua mambo mengi.... Wapo walio kuwa wanashika nafas za kwanza darasan ila leo Wanazidiwa uchumi na wenzao walio onekana hawana akili

4. Mwambie akifika chuo atakutana na watu wa mikoa tofauti na hata majiji. Ila akumbuke anatokea kijijini au wilaya iliyo duni, tena kule ndanindani... Hivyo asijikweze ili aonekane

5. Mwambie Marafiki wa chuo hubadilika kila baada ya semester. Kuendelea kung'ang'ania wale wa awali ataisoma namba....Akumbuke chuo ndiko mlokole hujifunza kwenda Club..kulewa na kuvaa nguo za ajabu

6. *Mwambie semester1 atakuwa na wapenzi wengi sana ila atumie kinga kwa gharama yoyote ile.* ..kama ni wakike akumbuke anasubiriwa na wale wa mwaka wa 2 na 3 ili asajiliwe ktk orodha ya Kontena jipya....

7. Mwambie makundi makundi chuoni humaliza hundi mfukoni... Atapata marafiki wapeta starehe. Pesa zake zitaisha

8. Mwambie Boom huwa linakuja ila Laki5 ya chuoni sio Laki5 ya nyumbani....hela ya chuoni huisha haraka na bila mpangilio hivyo awe makin ktk matumiz yake

9. Mwambie chuoni hakuna. NDOA ila kuna uzinzi.. Hivyo aachane kubeba majukum ya ndoa ikiwa kaenda kusoma. Mwambie kuishi kiunyumba na girl au boy kama wana ndoa sio ujanja ila ni ulimbuken na kesho ataumbuka

10. Mwambie awe na msimamo na asikurupuke kuanzisha mahusiano chuon ikiwa nyumban ana mtu anae mpenda kwa dhat.. Chuon kuna watu wapo kuharibu Malengo ya wengine awe makin

11. Mwambie wahadhiri (Lecturers) wa kitanzania wanatamaa ya ngono hivyo akiwa mvivu darasan bas atafeli na ili apewe Marks itabid awe tayar kumvulia chupi kila muhadhir ambao weng wao wagonjwa

12. Mwambie Chuoni kuna Makanisa na Misikiti. Wanafunzi ni zaidi ya 1000 lakini waumini ni wachache. Akumbuke kusali.

13. Mwambie kama ni wa kike kuwa aridhike na hali ya nyumban. Asifikirie kutafuta SPONSOR ili kupunguza ugum wa maisha .. Atajiingiza ktk matatizo makubwa

14. Mwambie kuwa   asiwadharau watu alio soma nao nyuma kisa hawajapata nafas kufika chuo.. Siku akimaliza chuo wapo atao wakuta wana biashara kubwa hivyo kumpa kibarua

15. Mwambie Simu na nguo za gharama ni muhimu lakini sio lazima... Hivyo asipende tumia vibaya pesa ambayo anapewa kwa awamu mana siku atazikumbuka akimaliza masomo

16. Mwambie marafiki wanaokuwa naye kipindi hana hela asiwasahau... Awaepuke marafik wanafik wanao mfundisha kutafuta wanawake au wanaume

17. Mwambie chuoni ni sehemu ya kutengeneza Connection na watu muhimu...akae mbali na watu wasio msaada kwake

18. Mwambie chuoni kuna watumishi wanao jiendeleza..husoma huku wakiendelea kupokea mshahara wengi wao ni waume na wake za watu.. Hawa ndo wanao tumia pesa zao kulaghai mabint na vijana

19.Mwambie pia baada ya kumaliza chuo haina maana amefanikiwa maisha. Hapa ndipo msoto mpya unapoanzia... Anapo waona kaka na dada zake wamemaliza chuo ila wapo tu mtaan asifikir ni wazembe ila usawa na mfumo unabana

20. Mwambie Maisha ni mafupi sana Adumu kumcha Mungu na kufanya mambo mazurii, Lastly Asimdharau mtu yeyote.,....Akumbuke na azingatie kuwa kuna maisha baada ya chuo...

Asijisahau sana maana mtaani kugumu.. Mabinti wenye DEGREE wana amua kuolewa na vibabu nao vijana kutembea na wazee sababu ya kukosa ajira....

Atambua kuwa leo hii dreva boda boda au bajaji ana uhakika wa kuilisha familia yake kila siku kuliko muhitimu wa chuo kikuu. Hivyo asiwe na dharau kuwa hawez olewa na mtu mwenye elimu ya chini

Pia akumbuke sio kila dreva au konda hajasoma..watu wana vyeti vyao na ufaulu mzur

Kama haelewi basi tumuache
Tumsubiri akimaliza.

IKIKUFAA IFANYIE KAZI
MUNGU AWAONGOZE KATIKA NJIA ILYOSAHIHI NA AWAPE UJUZI UTAKAOWASAIDIA ATA KAMA WATAKOSA AJIRA.
Ameen..
#enterprenuership
#invest_on_time.
#invest_for_ur_future

TANZANIA INA FURSA GANI ZA BIASHARA?

Habari,
Leo nakuletea Fursa za Biashara ambazo Tunaishi Nazo Tanzania,na wengi tumekua hatuzitumii.
    Zipo Fursa nyingi katika sekta mbalimbali kama; Kilimo,uchuuzi,usindikaji,kutengeneza bidhaa n.k
   Leo nakupa kwa uchache Fursa za biashara ndogondogo Tanzania ambazo unaweza kuzitumia na ukabadili maisha yako.

1.Kutengeneza Mifumo  inayotumia mtandao, (APPS) Mifumo hii inaweza kuwa mahususi kwa Huduma mbalimbali kama starehe/burudani,Biashara,Huduma za kijamii n.k

2.Ufugaji; hapa tunaangalia Ufugaji mdogo wa Mbuzi wa kisasa,kuku chotara,samaki,sungura,unenepeshaji ng'ombe n.k

3.Kilimo Biashara; Kilimo hiki kinategemea na hitaji la watu ila best ni "Mboga za Majani" hiki ni Kilimo ambacho soko lake ni kubwa Tanzania, pia unaweza kulima Papai,Tangawizi,Miche ya miti,n.k Kikubwa endana na uhitaji wa eneo ulilopo,

4.Usindikaji; Pia unaweza kusindika Asali,Viungo mbalimbali,Mafuta yatokanayo na matunda,n.k Chukua malighafi mtaani na uiongezee thamani kisha irudishe sokoni,

5.Huduma za usafiri; Katika kipengele hiki nitazungumzia juu ya kukodisha usafiri kama pikipiki au baiskeli kwa maeneo ya vijijini, na mijini, Kuwa wakala wa kampuni/mtu kutafuta wateja (Dalali) n.k

6.Huduma za Miamala ya simu; Hii ni Fursa Muhimu pia kuwa Wakala wa Tigo,Vodacom,Airtel n.k kuweka na kutoa fedha kusajili line na kutatua changamoto za mtandao,

7.Huduma ya kibanda umiza; Namaanisha kibanda cha kuonyeshea Movies,Mipira mbalimbali ya TPL,Afcon,EPL,UEFA n.k Pia katika kibanda hiki unaweza kuwa na Huduma za kucharge simu,kuuza vocha na kuuza vinywaji baridi

8.Huduma ya Genge; Genge pia huweza kubadili maisha yako tengeneza Genge uza mbogamboga kama, Dagaa, samaki,mchicha,ndizi,matunda mengne kama maembe,machungwa pia boresha uza mikate, n.k

9.Huduma ya Bites (mjini); Bites ni muhimu hasa maeneo ya stand za mabus unaweza tengeneza sehem ya kuuza vikorokoro mbalimbali vya kukaanga na uka make money, Hapa yaweza kuwa,Karanga,popcon,kuku,vusheti,crips,chips,n.k

10.Huduma ya maji,juice na urembo vituo vya mabus; Wapo wengi wanauza hivi vitu na ukitulia na kufanya Biashara vizuri hakika hutabeba lile boksi LA maji miaka miwili lazima uwe na mtaji

All the best
Kwa msaada Kibiashara nitafute hapa,
0710843184

Alhamisi, 8 Agosti 2019

FAIDA CHACHE ZA MWANAMKE MJAMZITO KUSHIRIKI TENDO LA NDOA

Kuna watu wamekua wakiuliza mara kwa mara kama inaruhusiwa kushiriki tendo la ndoa mpaka umri gani wa mimba au ni sahihi kufanya tendo la ndoa kipindi cha ujauzito? maswali yalikua mengi sana hivyo leo nimeamua nijibu maswali hayo na makala hii.
Mwanamke akiwa na mimba anaruhusiwa kushiriki tendo la ndoa hata kama anatarajia kuzaa kesho yake, hakuna tatizo lolote linalomzuia kufanya hivyo, baadhi ya wanawake wamekua wazito sana kufanya hivyo kwa kua na sababu mbalimbali za kujitetea bila kujua kwamba wanazikosa faida hizi ambazo ni muhumu kiafya. Faida zenyewe ni kama zifuatazo;

       Husaidia uchungu mzuri na kupona mapema;
Kufika kileleni wakati wa tendo la ndoa huambatana na kubana kwa misuli ya nyonga hii husaidia kuweka imara misuli ya nyonga ambayo ni muhimu sana wakati wa kusukuma mtoto na baada ya kuzaa kwani misuli hii ikiwa legevu mwanamke huweza kushindwa kuzaa kwa njia ya kawaida na hata baada ya kuzaa huweza kushindwa kuzuia mkojo usitoke wenyewe au kuvuja damu kwa muda mrefu.

       Hupunguza kwenda ovyo kukojoa au kujikojolea ;
Wakati wa ujauzito mtoto anapozidi kua mkubwa anazidi kukandamiza kibovu cha mkojo, hii humfanya mama aende chooni kukojoa mara kwa mara na wakati mwingine hata akipiga chafya au kukohoa basi mkojo unaweza kutoka wenyewe. tendo la ndoa huibana misuli ya nyonga na kuzuia hali hii.
      
       Huzuia uwezekano wa kupata kifafa cha mimba; Tafiti zinaonyesha kwamba aina ya protini inayopatikana kwenye mbegu za mwanaume huongeza kinga ya mwili na kuzuia uwezekano wa kupata kifafa cha mimba ambacho kinaua wanawake wengi sana.

       Hutibu tatizo la kufika kileleni kwa shida;
Kipindi cha ujauzito chuchu za mwanamke na kinembe chake huvimba na kuongezeka hisia mara dufu huku kiwango cha homoni za oestrogen kikiwa juu sana, hii humfanya kufika kileleni kirahisi sana kuliko mwanzoni.

       Huwapa uwezo wa kujiamini;
Kipindi cha ujauzito mwanamke hua anapata hofu sana na kutojiamini na mwili wake, hua na wasiwasi kwamba mwili wake unaharibika hivyo kitendo cha mwanaume wake kuendelea kushiriki naye tendo la ndoa humpa kujiamini kwamba mwili wake bado uko kwenye hali nzuri na anapendwa.

       Hupunguza msongo wa mawazo ; Kipindi cha ujauzito wanawake wengi huwaza sana kuhusu kesho yao…je swala la uchumi litakuaje? mwili wangu utakuaje? je ntapata jinsia nayotegemea? na kadhalika.. tendo la ndoa hutoa homoni ya upendo kwa jina la oxytocin, homoni hii hupunguza mawazo na kumpa amani mjamzito.
huongeza upendo na mshikamano kati ya wapenzi; Katika hali ya kawaida wanandoa wakikwazana wanaweza wakapatana kwa kushiriki tendo la ndoa tu, amani na upendo kipindi hiki ni muhimu sana kwani kuna mtoto anakuja ambaye anatakiwa kuzaliwa huku baba na mama wakiwa wanapatana.

       Hukuandaa na uchungu ; Ukishiriki ndoa wakati wa tarehe zilizokadiriwa zimefika unapata homoni moja kutoka kwenye mbegu za mwanaume kwa jina la prostglandin, homoni hii huivisha mlango wa uzazi na kuanza kufunguka taratibu kujiandaa na uchungu.
hutibu tatizo la kukosa usingizi ; Wanawake wengi wajawazito hua na dalili mbalimbali za maumivu na kuumwa sehemu tofauti za mwili na msongo wa mawazo, hii huweza kuwakosesha usingizi kabisa..tendo la ndoa huweza kuwapa usingizi mzuri.

       Hupunguza presha ya damu; Kipindi cha tendo la ndoa presha ya damu hushuka kwenye kiwango kizuri sana, hii ni muhimu sana kwa wanawake wenye hatari ya kupata kifafa cha mimba kama wanene sana, wenye kisukari au wenye historia za ugonjwa wa presha kwenye koo zao.
MWISHO;
Hakikisha unatumia staili za tendo la ndoa ambazo hazimuumizi mtoto na mama yaani hakikisha haulilalii tumbo hasa mimba ikiwa kubwa, kuna staili muhimu kipindi hiki kama kuangalia upande mmoja, mwanamke kuja juu, au mwanamke kuinama.

Jumatano, 7 Agosti 2019

AJABU YA MWANAMKE KISAIKOLOJIA Na.Hassan Issa

Wanawake ni binadamu wa ajabu sana katika uso huu wa Dunia yaani hawa watu ni next level, kuwaelewa ni ishu iliyowashinda hata wana falsafa, Newton na uwezo wake wote linapokuja suala la wanawake lazima atoke kapa na (ndio maana haieleweki hata kama akioa). Manabii na busara zao zote walishindwa kuwaelewa wakaishia kushauri ya kwamba tuishi nao kwa akili. Sasa najiuliza ni jambo gani unaweza fanya bila kutumia akili?, hapa ndipo napata ushahidi kwamba kumbe wanawake walishindikana tangu zama za mwanzo kabisa!. Wanasaikolojia wanasema kuwa kama utamuoa/kuishi na mwanamke  mwenye miaka 25 basi itakuchukua miaka 25 mingine kumuelewa huyo mwanamke angaalau kwa 90% maana hawa kila siku hubadilika na kuwa wapya kimatendo na kifikra.

Mwanamke unaweza mnunulia BMW X6 akatoka nayo kwenda kutembea, akiwa njiani akaombwa lift na kijana akampa akipitia sheli hela ya mafuta ikawa haitoshi, yule kijana akaamua kumuongeza ata elfu 20 basi mwanamke huweza kubadili mawazo na kumuona yule kijana ni bora kisa tu kachangia mafuta kuliko wewe uliyenunua BMW X6, mfano akitoka hapo akapitia supermarket kununua bidhaa labda akapungukiwa kiasi mfano anadaiwa elfu 20, na yule kijana akasema hiyo ntalipa mimi basi basi hapo atasahau zile zawadi zote huwa unambebea na hiyo elfu 20 inaweza kumfanya awaze kumtunuku yule kijana penzi.

Mwanamke unaweza mpa hela akanunue nyama kilo 5 buchani, mwenye bucha akimuongeza robo tu hilo litamfurahisha kiasi kwamba  anaweza kumpa mwenye bucha penzi na akusahau wewe ulieyota hela ya nyama kilo 5.

Mwanamke unaweza kumnunulia nguo, weaving, mafuta, perfume na urembo mzuri akavutia ila akipita mtaani akasifiwa na mwanaume kuwa kapendeza inaweza kuwa chanzo cha kumtunuku penzi na akakusahu wewe uliyegharamika na kufanya asifiwe!.

Mwanamke unaweza kumpa mimba na ukamhudumia mwanzo mwisho na familia ukalea kwa juhudi zako zote ila siku mkikosana anakwambia niache na watoto wangu, apo ashasahau kuwa wewe ndiye uliyempa mimba na kumlea yeye na watoto!

Mwanamke ndiye kiumbe pekee anayeweza kukupenda bila sababu ama kukuchukia bila sababu tofauti na viumbe wengine.

Mwanamke ndiye mwigizaji mkubwa ulimwenguni, anaweza kulia kwa furaha na akacheka kwa huzuni, bado hujawajua tu wanawake!

Mwanamke akisema ndio humaanisha hapana, na akisema hapana humaanisha ndio, pia anaweza kucheka bila kujua sababu lakini pia anaweza kulia pasipo sababu ya msingi ya kumfanya alie, hivyo chunga sana usijejichanganya!.

Mwanamke hupendi vutu vigumu na vyenye hatari mfano wanaume wenye nguvu, mlevi, muhuni (playboy), jambazi, mgomvi anayeogopwa hata na wanaume wenzie ila ukimuuliza anakuambia mie napenda kuwa na mwanaume mpole mwenye hofu ya Mungu tifauti na sisi wanaume tunavyopenda vitu vipole na vinyenyekevu na vyenye ukarimu, sasa wewe jifanye kumuamini mwanamke!

Jinsi unavyozidi kumpenda na kumthibutishia upendo wa dhati ndivyo unavyozidi kujiweka mbali nayeye, mwanamke hupenda migogoro isiyo na maana, ukijua hili ndoa haitokusumbua. Mwanamke hupendi utulivu kamwe!, usipomchokoa atakuchokoa tuu na usipomuendesha lazima akuendeshe yeye, Hawa viumbe hawana hiyana aisee!.

Mwanamke hupendi vitu vikubwa wala vidogo, kiufupi hana chaguo maalumu. Ukimnunulia gari sio garantii ya yeye kutulia nawewe bali anaweza kukusaliti hata na muosha gari wako. Ukimjengea nyumba nzuri na kumuwekea kila kitu sio njia ya kumteka kimahaba kwani anaweza kumtunuku penzi ata mtunza bustani wa nyumba yako.

Mwanamke hapendi ukweli, Ukimpa ukweli akija mwenye uongo basi we  andika maumivu. Unaweza kuwa na elfu 50 ukamueleza ukweli kuwa "mke wangu leo hali mbaya chukua hii elfu 30,"... akatokea jamaa akamuongopea kuwa "Chukua hii elfu 15 ngoja nimesahau ATM card yangu nyumbani ikifuka saa 10 jioni  ntakutumia laki 2 kwenye simu", Usishangae mkeo akakusaliti hata kabla ya hiyo saa 10 na iyo laki 2 asiione katu!.

Unamuoa hana ishu akiwa kwao amekaa tu,  unaamua kumfungulia biashara hata ya duka unamjazia kila kitu. anatokea mshikaji mmoja kumuunga pale dukani kila siku na kumuachia soda tu na hicho kinakuwa kigezo tosha cha kuona mshikaji anamjali kwa kumuachia ya soda kila siku kuliko wewe uliyemfungulia duka zima na kinachofuata ni usaliti tu.
😂🙌🏽🙌🏽🙌🏽🙌🏽
Huu ni utafiti mdogo wa Mtanzania mmoja

Jumatatu, 5 Agosti 2019

ISHI LEO YAKO KITAALAMU

Habari za Leo ndugu zangu, napenda kuwapa makala hii Leo ilikujifungua kidogo  pale tulipofungwa,
     Wengi tumechanganywa na Mada  Ya Leo na Tunajiuliza mmh  innocent anataka kusena mini? Au nitaishi vipi kitaalamu? Basi majibu ya maswali yako utayaoata hivi punde,
       Dunia ya leo nu Dunia iliyo jaa utandawazi, ni Dunia iliyo endelea pia tunasema ni Dunia iliyopiga hatua, Leo chochote ukitakacho unakipata tena kwa wepesi,
Swali; Nitaishije kitaalamu?.
Jibu lipo hivi;
1.Kuwa na ndoto inayo ishi katika maisha yako,
2.Anza kutengeneza njia za kufikia ndoto yako,
3.Jifunze zaidi namna ya kufikia malengo
4.Usikate tamaa juu ya ugumu unaoupitia.
5.Ishi kwa kufuata taratibu (mila na desturi) Za jamii inayo kuzunguka,(Jenga mahusiano mema)
6.Tatua matatizo ya jamii na yatumie kama fursa.(Tengeneza mtandao mzuri)
7.Tembea na kundi La watu wenye maono chanya,(Achana na mvuvu/mlalamikaji)
8.Zua mijadala ya kimaendeleo kukusanya fikra za wengine ili kutengeneza fursa,
9.Anza biashara yeyote kwa fedha yeyote uliyi nayo hata kama ni Kiduchu.
10.Fanya  tofauti na wengine kwa ubora zaidi,

Hayo ni baadhi ta Mambo Muhimu ambayo tunasema ni ya kitaalamu katika safari ya mafanikio yako.
  Hivyo nikutakie utekelezaji mzuri wa hayo machache na endelea kufuatilia makala zangu ujifuuze zaidi,
*ishi kitaalamu usiishi kizembe (Kivivu)*
Ni Mimi Mwalimu wako Innocent M Priscus,

NAMNA NZURI YA KUANDAA MPANGO WA BIASHARA


Biashara zote nzuri zinahitaji mpangilio. Panga vyema na utatengeneza pesa zaidi. Mpangilio wa biashara unakufanya uangazie malengo yako makuu. Unakutaarifu ulikotoka, umefikia wapi kwa sasa, na ni wapi unahitaji kuenda kama biashara.
Inaweza pia kukusaidia kupata mkopo kutoka benki, inasaidia watu kukukopesha pesa na inawaeleza watu unataka biashara yako iwe vipi katika muda wa miaka 3 mpaka 5.
Hatua ya

1: Muhtasari na maelezo ya biashara.
Moja ya vitu vya kwanza unachohitaji kufanya ni kuandika muhtasari wa biashara na maelezo. Hii itakusaidia wewe na wengine kuelewa nini unachotarajia kufanikisha:
Muhtasari wa Biashara : Nini unataka kufanya? Wapi? Vipi? Kwa kiasi gani?
Maelezo ya Biashara : Nini kinatokea leo? Nini kinaweza kutokea hapo mbeleni katika eneo lako? Unaweza kufanya nini? Unaweza kuifanya vipi? Kitatengeneza vipi pesa?

Hatua ya 2: Mpango wa uzalishaji
Hakikisha muda wote una kitu cha kuuza kwa mfano ng’ombe wa maziwa. Kama ng’ombe wako wote watazaa kwa wakati moja, hautakua na maziwa ya kuuza. Kama una ng’ombe mmoja anaetoa maziwa, nini kitatokea kama akiwa mgonjwa?
Mara nyingine ni vizuri kuwa na biashara zaidi ya moja. Jaribu kufuga kuku au kupanda mboga.

Hatua ya 3: Mpango wa Masoko
Angalia soko. Nini kinatokea katika soko kwaajili ya biashara yako leo? Hatua muhimu ni kutambua mnunuzi kwaajili ya zao lako, kuhakikisha unahudumia kuendana na mahitaji. Hii itahakikisha unapata rejesho katika uwekezaji wako.
Kuna Ushindani gani hapo? Kama una mshindani, unahitaji kufikiria jinsi unavyoweza kuwa tofauti na kutoa thamani nzuri kwa wateja wako. Utafanya nini kama mshindani akitokea?
       Zingatia P 4 zifuatazo – Bei, Bidhaa, Ukuzaji na Mahali:
Uza kwa bei nzuri. Tambua kiasi majirani zako wanachouzia maziwa. Kama bei iko juu sana watu hawatanunua maziwa yako.
Bidhaa yako ni gani? Katika hili je maziwa ni safi na mabichi( Haijakaa).
Watu wanajuaje kama unauza maziwa? Unahitaji kutangaza . Bango/ Tangazo mlangoni? Kuwajulisha watu kanisani?
Wapi watu wanaweza kununua maziwa yako? Nyumbani kwako? Unapeleka? Kwenye OLX au mtandao wa kijamii?
Kwa taarifa zaidi kuhusu kujua masoko bonyeza hapa.
Hatua ya

4: Mpango wa kifedha.
Uzalishaji na utafutaji masoko unagharimu pesa. Unahitaji kiasi gani cha fedha? Je utahitaji mkopo? Una akiba ambazo unaweza kutumia?
Utahitaji kuandaa bajeti. Panga bajeti yako kukopa, kuweka akiba, kuwa na pesa za kuendesha na kukuza biashara yako, na kiasi gani unaweza kujilipa.

Hatua ya 5: Mpango wa kuendesha biashara
Jinsi gani biashara itaendeshwa siku baada ya siku? Je utahitaji watu wa kukusaidia? Je utahitaji kufanyia ukarabati vifaa vyako na je unahitaji usafiri?

Hatua ya 6: Mkadirio ya hatari
Matatizo inaweza kutokea wapi? Ni muhimu kuwaza kwa kina kuhusu hatari , kwa mfano; Utafanya nini kama mavuno ya mazao yako ni mabaya na kama ng’ombe wako akiwa mgonjwa