Jumatano, 30 Oktoba 2019

UJUMBE MFUPI WA LEO Na, Mwl Massawe

Mwanaume mmoja alimuoa mwanamke mrembo na alikuwa akimpenda sana. Siku moja huyo mwanamke alipatwa na maradhi ya ngozi hivyo kidogo kidogo alianza kupoteza urembo wake.

Mume alipata safari na wakati akirudi alipata ajali iliyomfanya apoteze uwezo wake wa kuona. Hata hivyo, maisha yao ya ndoa yaliendelea kama kawaida. Lakini kadiri siku zilivyosonga mbele ndivyo mke alivyoendelea kupoteza urembo wake. Kwa kuwa mume alikuwa kipofu hakulijua hilo na hivyo hakuna kilichobadilika kwenye upendo wao. Aliendelea kumpenda na mke alimpenda sana mumewe.

Siku moja mke wake alifariki dunia. Ilikuwa huzuni kubwa sana kwa mume. Baada ya kumaliza taratibu zote za maziko, mazishi na kutandua msiba, alipanga kuhama kwenye mji huo na kwenda kuishi kwenye mji mwingine.

Mtu mmoja aliposikia habari hiyo alimwendea na kumuuliza: _“Sasa utawezaje kutembea peke yako? Maana siku zote hizi mkeo alikuwa akikusaidia kukuonesha njia.”_

Akajibu: _“Mimi si kipofu. Nilifanya ionekane hivyo kwa sababu angejua kwamba ninauona mwili wake ulivyobadilika kuwa mbaya angepata maumivu makubwa zaidi kuliko ugonjwa wake wenyewe. Alikuwa mke mwema sana. Nilitaka aendelee kuwa na furaha.”_

*FUNZO:*

_*Wakati fulani ni vizuri ukajifanya kipofu na kuyapuuza mapungufu ya mwenzako ili kumfanya awe mwenye furaha.*_

Meno huung’ata ulimi mara nyingi, lakini vinaendelea kuishi pamoja kinywani. Huo ndio moyo wa *KUSAMEHEANA.* 

Macho hayaonani, lakini yanatazama na kuona vitu kwa pamoja, hupepesa na kulia pamoja. Huo unaitwa *UMOJA.*

1. Ukiwa peke yako unaweza kuongea, lakini ukiwa pamoja na mwenzako mnaweza *KUZUNGUMZA.*

2. Ukiwa peke yako unaweza *KUFURAHI,* lakini ukiwa na mwenzako unaweza *KUFURAHIA.* 

3. Ukiwa peke yako unaweza *KUTABASAMU,* lakini ukiwa na mwenzako mnaweza *KUCHEKA.*

Huo ndio *UZURI* wa mahusiano yetu kama binadamu. Tunategemeana. 

Kiwembe kina ukali lakini hakiwezi kukata mti; shoka lina nguvu na imara lakini haliwezi kukata nywele.

*Kila mtu ni muhimu kulingana na kusudio na lengo la uwepo wake. Usimdharau mtu yeyote kwa hali yoyote, kwa sababu huwezi kuwa yeye.*

*Mwenyezi Mungu atujaalie nguvu na moyo wa kusamehe, kustahmiliana na kuishi kwa upendo na umoja.*

Jumamosi, 26 Oktoba 2019

FAHAMU UWEZO WA NDEGE MPYA YA ATCL (Boeing 787 Dreemliner) KUTOKA NCHINI MAREKANI

Kwa kifupi ndege hii mpya iliyowasili Leo ina uwezo ufuatao

1*Ina uwezo wa kubeba jumla ya abiria 262
2*Ndege hiyo pia ina uwezo wa kubeba uzito wa tani 227. Uzito huo unajumuisha chombo, mizigo na mafuta. Sifa yake ni kwamba ina uwezo wa kuhimili hali nzito ya hewa ikiwa kwenye umbali mrefu kwenda juu.
3*Inabeba Lita 101,000 za mafuta na ukubwa wa mita 56.72 sawa na nusu ya uwanja wa mpira wa miguu.
Vilvile ndege hiyo ina uwezo wa kutembea kilomita 13620 sawa na saa zaidi 12 hewani bila ya kusimama

Alhamisi, 17 Oktoba 2019

HOW TO SUCCEEDED IN LIFE (Quote)

Infuse your life with action. Don't wait for it to happen. Make it happen. Make your own future. Make your own hope. Make your own love. And whatever your beliefs, honor your creator, not by passively waiting for grace to come down from upon high, but by doing what you can to make grace happen... yourself, right now, right down here on Earth

MAMBO MATANO YANAYOWEZA KUFUPISHA MAISHA YAKO, (Kusababisha uishi umri mfupi)

       Kwa kawaida maisha ya kibinadamu mwisho wake huwa ni kufa, hivyo kila mwenye pumzi hii leo mwisho wa maisha yake huishia kaburini.
Hata hivyo, kumekuwepo na viashiria fulani fulani ambavyo huweza kuashiria baadhi ya makundi fulani ya watu huenda wanaweza kuwa na muda mfupi wa kuishi duniani kutokana na sababu tofauti tofauti.
Miongoni mwa dalili ambazo huweza kuashiria mhusika anaweza kuwa na maisha mafupi duniani ni pamoja na hizi zifuatazo.

       1. Watu wenye kupenda maisha ya anasa na starehe
Watu wa aina hii huwa katika hatari ya kupoteza maisha haraka hata kabla ya siku zao kutokana na kuwa na hatari kubwa ya kupatwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo ya zinaa.

       2. Wavutaji wa sigara.
Watu wanaovuta sigara huwa katika hatari ya kuishi maisha mafupi zaidi kuliko wale ambao hawatumii sigara kwani watu wa aina hii huwa katika hatari ya kukumbwa na saratani ambayo huweza kukatisha uhai wa mhusika hata kabla ya siku zake.

       3. Kushinda umekaa siku nzima
Wale ambao huwa miili yao haina mazoezi kabisa nao huwa katika hatari ya kupoteza maisha mapema kutokana na kushambuliwa na magonjwa yasiyoambukiza kama vile shinikizo la damu, kisukari nk.
     
       4. Unywaji wa pombe
Watumiaji wa vileo na huwa katika hatari ya kupoteza maisha yao mapema kutokana na mambo mawili makuu
a) Kupata ajali kutokana na kutumia vyombo vya moto wakati wakiwa wamelewa na baadaye kujikuta wanapoteza maisha.
b) Ugomvi ambao huweza kuibuka kutokana na mihemko ya vilevi wanavyokuwa wamekunywa na kuweza kusababisha ugomvi mkubwa. Mfano kupigana na chupa na baadaye kupoteza uhai.

        5. Ulaji wa vyakula vya viwandani
Kuna wale ambao mara nyingi wamekuwa wakila vyakula vya makopo ambavyo vinapotumiwa mara kwa kwa mara huweza kuwa na madhara kadhaa likiwemo tatizo la saratani. Hivyo kundi hili nalo linaweza kuwa katika hatari ya kupoteza maisha kabla ya siku zao

Jumanne, 15 Oktoba 2019

MAJINA YA WANAFUNZI KUMI BORA WALIOFAULU MTIHANI WA DARASA LA SABA 2019

Hawa ndio wanafunzi vinara katika matokao ya mtihani wa darasa La saba mwaka 2019, kwa matokeo zaidi bofya link hapo,

https://results.necta.go.tz/results/2019/psle/psle.htm


Matokeo haya yametoka tarehe 15/10/2019 na kanda ya ziwa waibuka kuwa na matokeo mazuri zaidi,

MIKOA KUMI 10 BORA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2019

   Hii ndiyo mikoa iliyofanya Vizuri katika matokeo ya darasa la saba Leo tarehe 15/10/2019,

MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA 2019,

https://results.necta.go.tz/results/2019/psle/psle.htm       Dar es Salaam. Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kumaliza elimu ya msingi mwaka 2019 ambapo asilimia 81.50 ya watahiniwa 933,369 wamefaulu mtihani huo huku watahiniwa 909 wakifutiwa matokeo kwa sababu ya udanganyifu.
MATOKEO YOTE BONNYEZA HAPA
Akitangaza matokeo hayo leo Jumanne Oktoba 15, 2019 Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk Charles Msonde amesema kwa jumla yanaonyesha ufaulu umeongezeka kwa asililia 3.78 lakini ufaulu katika somo la Kiingereza bado ni mdogo likilinganishwa na masomo mengine.
"Ufaulu katika somo la Kiingereza unaendelea kuimarika mwaka hadi mwaka hivyo juhudi za makusudi zinahitajika kuendelea kufanyika ili kuinua kiwango cha ufaulu katika somo hili," amesema Dk Msonde.
         Aidha katika matokeo hayo, Grace Imori Manga wa shule ya msingi Graiyaki ya mkoani Mara ametangazwa kuwa wa kwanza kitaifa akifuatiwa na Francis Gwani wa shule ya msingi Paradise ya mkoani Geita na namba tatu imeshikiliwa na Loi Kitundu wa Shule ya msingi Mbezi ya Dar es Salaam.
         Wengine katika orodha ya 10 bora ni Victor Godfrey wa shule ya msingi Graiyaki, Azizi Yassin wa Graiyaki goldie Hhayuma wa Graiyaki, Daniel Daniel wa shule ya msingi Little Mkoani Shinyanga, Hilary Nassor wa Peaceland ya Mwanza, Mbelele Mbelele wa Kwema Modern ya Shinyanga na Nyanswi Richard wa Graiyaki ya Mara.
         Shule 10 bora kitaifa ni Graiyaki ya Mara, Twibhoki ya Mara, Kemebos ya Kagera, Little Treasures ya Shinyanga, Musabe ya Mwanza, Tulele ya Mwanza, Kwema Morden ya Shinyanga, Peaceland ya Mwanza, Mugini ya Mwanza na Rocken Hill ya Shinyanga.
Kimkoa, Mkoa wa Dar es Salaam umeshika namba moja ukifuatiwa na Arusha, Iringa, Kagera, Katavi, Kilimanjaro, Mbeya, Simiyu, Njombe na Pwani.
Halmashauri 10 bora zimeongozwa na Arusha jiji, Ilemela, Kinondoni, Mwanza jiji, Ilala Manispaa, Moshi Manispaa, Bukoba Manispaa, Iringa Manispaa, Biharamulo na Arusha
       
https://results.necta.go.tz/results/2019/psle/psle.htm

KAULI TANO ZA KUKUONGOZA UNAPOKUA KAZINI

Kila kazi ina muda na wakati wake kabla hujaanza kazi asubuhi jaribu kupitia haya kwa makini 

 A,Kuna maisha baada ya kazi unayoifanya, heshimu kipato chako na usimdharau mtu kwa nafasi uliyonayo,

 B,Fanya jambo kwa nafasi yako siyo kwa kuiga, angalia nafasi yako katika kusaidia na kufanya kitu Fulani,Kama mwenzako kafanya makubwa na huna uwezo was kufanya kama yeye usilazimishe,

 C.Penda kazi yako angalia ulipotoka na usifuate makundi, kumbuka kazi uliomba mwenyewe na ukafika mwenyewe marafiki uliowakuta kazini wasibadili tabia yako na kukufanya upotee kwani mwisho wa Sik kila mmoja atarudi alipotoka,

 D.Busara yako ikuongoze katika mambo yako kazini, kabla hujachangia chochote fikiria kwanza ubora na udhaifu was kile unachoenda kukiongea ndipo utoe hoja kukosoa au kuunga mkono,

 E. Tii mamlaka iliyoko juu yako, tii viongozi wako na Fanya kazi pasipo kuangalia udhaifu wao kwani hata maandiko matakatifu yanasema tiini mamlaka iliyo kuu kwani mamlaka zote zimewekwa na Mungu,

Kwa elimu na mafunzo mbalimbali ya namna ya kufanikiwa tucheki SMS/WhatsApp no: 0710843184
Mwl Innocent Massawe Priscus

HISTORIA YA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE (BABA WA TAIFA)

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa raisi wa kwanza wa Tanzania, alizaliwa Butiama mkoani Mara mnamo tarehe 13 April 1922 na alifariki dunia 14 Oktoba 1999.
Alikuwa mojawapo kati watoto 26 wa Nyerere Burito, chifu wa kabila la Wazanaki. Alipokuwa mtoto Nyerere alichunga mifugo ya babake; katika umri wa miaka 12 aliingia shule akitembea kilomita 30 hadi Musoma. Baada ya kumaliza shule ya msingi aliendelea kusom
a shule ya wamisionari Wakatoliki huko Tabora. Katika umri wa miaka 20 alibatizwa akawa mkristo Mkatoliki hadi mwisho wa maisha yake.
(Mama Maria Nyerere, mke wa Hayati baba wa Taifa)
Mapadre wakaona akili yake wakamsaidia kusoma ualimu huko Makerere, Kampala, Uganda kuanzia 1943 - 1945. Makerere akaanzisha tawi la Umoja wa wanafunzi Watanganyika pia amejihusisha na tawi la Tanganyika African Association (TAA). Baada ya kumaliza masomo ya ualimu alirudi Tabora akifundisha shule ya St.Mary´s. Mwaka 1949 alipata skolashipu ya kwenda kusoma kwenye Chuo Kikuu cha Edinburgh huko Uskoti / Uingereza akasoma M.A. ya historia na uchumi(alikuwa mtanzania wa kwanza kusoma katika chuo kikuu cha Uingereza na mtanzania wa pili kupata shahada ya elimu ya juu nje ya Tanzania).
Aliporejea Tanganyika kutoka masomoni, Nyerere alifundisha Historia, Kingereza na Kiswahili katika shule ya St. Francis iliyo karibu na Dar es Salaam. Mwaka 1953 alichaguliwa kuwa raisi wa chama cha Tanganyika African Association (TAA), cham
a ambacho alikisaidia kukijenga alipokuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha Makerere. Mwaka 1954 alikibadilisha chama cha TAA kwenda katika chama cha Tanganyika African National Union (TANU) ambacho kilikuwa cha kisiasa zaidi kuliko TAA. Ndani ya mwaka mmoja chama cha TANU kilikuwa tayari chama cha siasa kinachoongoza Tanganyika.
Uwezo wa mwl. Nyerere uliwashitua uongozi wa kikoloni na kumlazimisha Nyerere kuchagua kati ya siasa na kazi ya ualimu. Nyerere alisikika akisema kuwa alikuwa mwalimu kwa kuchagua na mwanasiasa kwa bahati mbaya. Alijiuzuru ualimu na kuzunguka nchini Tanganyika kuzungumza na watu wa kawaida na machifu ili kuleta muungano katika mapigano ya uhuru. Pia alizungumza kwa niaba ya TANU katika Trusteeship council na Fourth committee ya Umoja wa Mataifa (UN) huko New York. Uwezo wake wa kimaongezi na kuunganisha watu ulimwezesha kufanikisha Tanganyika kupata uhuru bila umwagaji wa damu.
Ushirikiano mzuri aliouonyesha aliyekuwa gavana wa wakati huo bwana Richard Turnbull ulisaidia pia kuharakisha upatikanaji wa uhuru. Nyerere aliingia katika bunge la kikoloni mwaka 1958 na kuchaguliwa kuwa waziri mkuu mwaka 1960. Mwaka 1961 Tanganyika ilipata uhuru wake na tarehe 9/12/1961 Nyerere alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa Tanganyika huru na mwaka mmoja baadae Nyerere alikuwa raisi wa kwanza wa jamhuri ya Tanganyika. Nyerere alikuwa kiungo muhimu katika katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutengeneza Tanzania baada ya mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 yaliyomtoa madarakani sultani wa Zanzibar Jamshid bin Abdullah.
Sifa zake
Bado anakumbukwa na watanzania hasa wa hali ya chini kutokana na sera zake za kujali utu na ubinadamu.Pia ataendelea kukumbukwa na waafrika kote barani hasa kwa mchango wake mkubwa wakati wa harakati za kupigania uhuru katika nchi mbali mbali barani Afrika.
Ni mmoja wa viongozi wachache wanaokumbukwa kwa kutojilimbikizia mali pamoja na kutawala kwa miaka zaidi ya 24.
Mwishoni mwa maisha yake Nyerere aliishi kama mkulima wa kawaida kijijini kwake Butiama. Alipatwa na kansa ya damu (leukemia) na kufariki Uingereza wakati wa kutibiwa katika mji wa London tarehe 14 Oktoba, 1999. Alizikwa mahali pa kuzaliwa kwake, kijiji cha Butiama.
(Kaburi la Baba wa Taifa)
Watanzania tumempoteza kiongozi mpiganaji na mwenye uchungu na nchi yake, aliepinga vita dhidi ya umasikini, ubaguzi na rushwa. Hamna kiongozi mwengine alieiga mfano wa Baba wa Taifa tumebakiwa na viongozi wenye uchu na madaraka kujirumbukizia mali wao na familia zako ni aibu sana kwa Taifa maana enzi za Mwalimu hapakukuwa na hali hii ya kiongozi kumiliki mali nyingi mfano mzuri alionesha yeye ambae hakuwa na uchu wa kujirumbikizia mali ingawa alikuwa na nafasi kubwa na inayomfanya aweze kufanya hivyo lakini alikuwa na uzalendo na nchi yake. Nchi sasa inapoteza dira hamna viongozi bora ila kuna bora viongozi aibu kwa Watanzania.

AINA ZA WATU NA TABIA ZAO KATIKA KIPATO NA MAFANIKIO

Jitambue upo katika nafasi gani.
    Leo nakuletea aina tatu za watu katika tofauti katika kipato pamoja na tabia zao,
,Katika maisha yetu ya kila Siku tuna aina tatu za watu kulingana na kipato chao ambao ni hawa wafuatao;
  A,Watu wenye kipato cha juu,
  B,Watu wenye kipato cha kati,
  C,Watu wenye kipato cha chini,
Hayo ndiyo makundi makuu ya kipato katika Dunia hii ya Teknolojia, Kiufupi tutazame sifa/tabia za kila kundi,

                  A.WATU WENYE KIPATO CHA JUU;
 za hawa hutumia kipato walichonacho kuzalisha kipato kingine, Mfano anamoliki Kampuni kubwa fedha anazozipata huzitumia kufungua kampuni nyingine ndogo.
      Pia hawa huweka akiba na kwa kawaida huendelea kukua na kufanikiwa zaidi kutokana na kuwa na vyanzo vingi vya mapato,
     Tabia nyingine huwa ni wavumilivu, wenye subira, wanajali na wapo makini katika kusimamia miradi yao vilevile wana uhusiano mzuri sana na jamii inayo wazunguka,
      Tabia ya mwisho watu hawa hutumia muda wote 24 hrs kuzalisha na huwa na dharura nyingi wanapo alikwa katika sherehe au matamasha kutokana na huwa bize sana,

                B.WATU WENYE KIPATO CHA KATI
Hawa tunao kwa wastani katika mazingira yetu na huwa wana tabia zinazo shabihiana na za wale wenye kipato cha juu na maranyingi huweza kufikia kipato cha juu kirahisi, Hawa hupenda kuzalisha Mali pia baadhi hupenda starehe za wastani na muda mwingi huutumia katika kuzalisha na starehe, ni rahisi sana hawa kutajirika pia ni rahisi kufilisika,
      Katika hatua hii wengi huwekeza katika asset mbalimbali kama mashamba/viwanja nyumba/majengo n.k

                C.WATU WENYE KIPATO CHA CHINI
Hawa ndio wenye kundi kubwa Duniani, watu hawa wana sifa nyingi zinazowafanya kuendelea kuwa maskini;
1.Wavivu kufanya kazi na hupenda kuajiriwa kuliko kujiajiri wenyewe hulala sana na hupenda starehe, hunununa mapambo mengi ya ndani na vikorokoro vingi vya nyumbani,pia hawana akiba na hufanya matumizi makubwa bila mipango, humiliki vitu vya anasa visivyozalisha kama nguo,n.k
2.Kwakawaida watu hawa hawatumii kipato chao kuzalisha kipato kingine hivyo hubaki katika umasikini wao daima,

MWISHO; Kila mtu alizaliwa maskini lakini siyo kila MTU atakufa maskini, hii ni kutokana na mfumo wa maisha yako, Badili mtazamo wako sasa na Ishi kitaalamu ukiiona kesho iliyo bora kuliko Leo,
Kwa msaada wa kijasiriamali wasiliana nasi
0710843184/0753352264
Mwl wako INNOCENT M PRISCUS

Jumapili, 13 Oktoba 2019

SIKU TATU ZAONGEZWA KATIKA UANDIKISHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA


WAZIRI wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo ameongeza siku tatu kwa wananchi kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24 Mwaka huu.
Jafo awachongea Ma-RC kwa Rais
Stars kamili yawasili Kigali
MCT yaboresha tuzo uandishi wa habari
Mvua zasababisha madhara makubwa HABARI KUBWA Akizungumza kabla ya kujiandikisha Kijijini kwake Kimani,Kisarawe mkoani Pwani leo, Waziri Jafo alisema kuongezwa kwa siku tatu hizo kumetokana na sababu mbalimbali ambazo kimsingi zimesababisha wananchi kuikosa fursa hiyo.
Alisema kimsingi siku za uandikishaji huo zilizoongezwa kutoka leo hadi Oktoba 17, kumesabishwa na tatizo la mvua zinazoendelea kunyesha katika mikoa mbalimbali na hivyo kuleta shida kwa wananchi wengi kujiandikisha.
Aliitaja sababu nyingine kuwa ni pamoja na uwepo wa zoezi la wananchi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura, hali iliyoleta dhana kwa baadhi ya wananchi kuwa kitambulisho cha mpiga kura kitawawezesha kupiga kura katika uchaguzi huo wa Serikali za mitaa.
"Kutokana na sababu hizo na kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa za Mwaka 2019 na matangazo ya Serikali Na 371,372,373 na 374 ya Mwaka 2019 Waziri mwenye dhamana na Serikali za mitaa ana mamlaka ya kutoa miongozo mbalimbali kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa" alisema Jafo
Alisema kutokana na kanuni hizo na changamoto zilizojitokeza Wizara yake imeona vyema kuongeza siku hizo tatu ili kuwapa nafasi wananchi kujiandikisha na hivyo kutumia fursa yao ya kikatiba kuwachagua viongozi wanaowataka.
Aidha alisema tangu kuanza kwa Oktoba 8 hadi Octoba 12 Mwaka huu wananchi zaidi ya Milioni 11 walikuwa tayari wamejiandikisha nchi nzima kushiriki uchaguzi huo huku akilitaja zoezi hilo kuwa lenye mafanikio makubwa ikilinganishwa na kipindi kingine chote.
Alisema kufuatia mabadiliko, ratiba ya uandikishaji wa orodha ya wapiga kura na matukio yanayohusu uandikishanji yatakuwa na mabadiliko fulani fulani ikiwemo kubandikwa kwa orodha ya wapiga kura litakalofanyika kuanzia Oktoba 18, utoaji wa pingamizi kuhusu uandikishaji wapiga kura litakalofanyika Oktoba 14 hadi 24.Mabadiliko mengine ni pamoja na uamuzi kuhusu pingamizi litalofanyika kuanzia Oktoba 24 hadi 25,marekebisho ya orodha ya wapiga kura kuanziaa Oktoba 25 hadi 25 pamoja na ukataji wa rufaa dhidi ya uamuzi wa pingamizi utakaofanyika Oktoba 24 hadi 26 sambamba na ukataji wa rufaa utakaofanyika Oktoba 24 hadi 29 Mwaka huu.
Aidha alisema matukio mengine yote zikiwemo kampeni za wagombea zitaendelea kubaki kama kawaida huku akiwataka wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili kuwa na sifa ya kupiga kura katika uchaguzi huo. 13 OCT 2019

NAMNA YA KUMFURAHISHA MPENZI WAKO

TENDO la ndoa (kwa wanandoa) si tu linatumika kuboresha uhusiano kati ya mume na mke bali pia ni dawa inayoweza kuutibu mwili, akili na hisia. Hata hivyo, lazima liwe ni tendo lililokamilika, kwa maana lazima mwanaume na mwanamke wote walifurahie na kuridhika.
Tendo hili lisipofanyika kwa ukamilifu wake, hubadilika na kuwa kero kubwa na janga kwa wanandoa. Kama ambavyo nimekuwa nikieleza mara kwa mara, sidhani kama yupo mtu ambaye hataki kumfurahisha mwenzi wake wawapo faragha.
Tatizo ni kwamba wengi hawana maarifa ya nini cha kufanya awapo faragha na mwenzi wake, na matokeo yake wamekuwa wakijiendea wanavyoweza, kama kutembea kwenye giza totoro usiku wa manane.
Hakuna mahali ambapo unaweza kufundishwa namna ya kumfurahisha mumeo au mkeo, angalau kidogo wazee wetu enzi zao walikuwa wanapelekwa jandoni na unyagoni, siku hizi unakuja kujifunzia ndani ya ndoa, yaani kama ni mechi ya mpira wa miguu basi unajifunzia kutuliza mpira na kupiga danadana uwanjani wakati wa mechi ambayo ni lazima ushinde.
M f a n o mwepesi ambao huwa napenda kuutumia ni kwamba kila mtu anaweza kuwa anatamani kupiga gitaa na kuzalisha muziki mzuri, lakini hebu jiulize, kama hujawahi kujifunza kupiga gitaa na ukaelewa, ukipewa gitaa sasa hivi unaweza kupiga na kutoa muziki mzuri? Jibu ni HAPANA.
Mapenzi ni sanaa, lazima ukubali kujifunza na kuyatafuta maarifa mahali popote yalipo ili uwe bora, huyo uliyenaye unaweza kuwa unafanya kila kitu kwa ajili yake, unajitahidi kumuonyesha upendo wa hali ya juu lakini kama hujui nini cha kufanya muwapo faragha ili afurahi, ni sawa na kazi bure. Ni kwa msingi huo ndiyo maana nikaamua tujadiliane mada hii kama inavyojieleza hapo juu.
MAANDALIZI YA KIHISIA
Jambo la kwanza ambalo unatakiwa kulifahamu, ni kwamba ili mume au mke afurahie tendo muwapo faragha, lazima awe ametulia kihisia. Haiwezekani mmetoka kukwazana kuhusu jambo fulani, hamjapata suluhu na kila mmoja ana hasira halafu ndiyo mnaingia uwanjani, hamuwezi kufurahia tendo kwa mtindo huo na hii inawahusu wote.
Maandalizi mazuri ya tendo yanaanzia katika maelewano, mpokee vizuri kwa maneno yaliyojaa bashasha, kwa sauti ya upole, mbembeleze, mpeti­peti na msifie! Ukiikamilisha kwa ukamilifu hatua hii ya kwanza na ya muhimu, basi utakuwa tayari umeshamuingiza kwenye safari ya kuelekea kufurahia tendo.
Mnapokuwa eneo la tukio, hutakiwi kuwa na papara! Lazima kwanza na wewe akili yako uitulize na badala ya kukimbilia kuingia mchezoni na kuanza kupiga mbizi kama mtu anayejifunza kuogelea, unatakiwa kwanza kutumia muda wa kutosha kupasha misuli moto.
Muda unaoshauriwa kitaalamu, ni angalau dakika thelathini
ndani ya muda huu mfanyie yale mambo yatakayoamsha hisia zake za ndani, viungo vya mwili wako kama mikono, vidole, mdomo, masikio vinaweza kuzalisha hisia nzuri sana kama utakuwa unajua nini unatakiwa kufanya kwa wakati gani.
Narudia tena, epuka kuwa na papara za kukimbilia uwanjani, maandalizi ni muhimu sana kwani yatamuandaa mwenzi wako kimwili na kihisia. Ukiwa na uhakika kwamba maandalizi yamefanyika kwa ukamilifu, sasa unaruhusiwa kuendelea na hatua kubwa na ya muhimu inayofuatia.
Katika hatua hii ambayo kimsingi ndiyo inayowaunganisha, pia unatakiwa kuwa na uelewa juu ya nini cha kufanya na kwa mtindo gani, siyo un­aingia kwa papara kama unakimbizwa, hapana. Hapa pia unatakiwa kujifunza zaidi ili kuhakikisha unaibuka mshindi kwa kumfikisha mwenzi wako kwenye kilele cha safari yake ya huba.