Jumatano, 30 Oktoba 2019

UJUMBE MFUPI WA LEO Na, Mwl Massawe

Mwanaume mmoja alimuoa mwanamke mrembo na alikuwa akimpenda sana. Siku moja huyo mwanamke alipatwa na maradhi ya ngozi hivyo kidogo kidogo alianza kupoteza urembo wake.

Mume alipata safari na wakati akirudi alipata ajali iliyomfanya apoteze uwezo wake wa kuona. Hata hivyo, maisha yao ya ndoa yaliendelea kama kawaida. Lakini kadiri siku zilivyosonga mbele ndivyo mke alivyoendelea kupoteza urembo wake. Kwa kuwa mume alikuwa kipofu hakulijua hilo na hivyo hakuna kilichobadilika kwenye upendo wao. Aliendelea kumpenda na mke alimpenda sana mumewe.

Siku moja mke wake alifariki dunia. Ilikuwa huzuni kubwa sana kwa mume. Baada ya kumaliza taratibu zote za maziko, mazishi na kutandua msiba, alipanga kuhama kwenye mji huo na kwenda kuishi kwenye mji mwingine.

Mtu mmoja aliposikia habari hiyo alimwendea na kumuuliza: _“Sasa utawezaje kutembea peke yako? Maana siku zote hizi mkeo alikuwa akikusaidia kukuonesha njia.”_

Akajibu: _“Mimi si kipofu. Nilifanya ionekane hivyo kwa sababu angejua kwamba ninauona mwili wake ulivyobadilika kuwa mbaya angepata maumivu makubwa zaidi kuliko ugonjwa wake wenyewe. Alikuwa mke mwema sana. Nilitaka aendelee kuwa na furaha.”_

*FUNZO:*

_*Wakati fulani ni vizuri ukajifanya kipofu na kuyapuuza mapungufu ya mwenzako ili kumfanya awe mwenye furaha.*_

Meno huung’ata ulimi mara nyingi, lakini vinaendelea kuishi pamoja kinywani. Huo ndio moyo wa *KUSAMEHEANA.* 

Macho hayaonani, lakini yanatazama na kuona vitu kwa pamoja, hupepesa na kulia pamoja. Huo unaitwa *UMOJA.*

1. Ukiwa peke yako unaweza kuongea, lakini ukiwa pamoja na mwenzako mnaweza *KUZUNGUMZA.*

2. Ukiwa peke yako unaweza *KUFURAHI,* lakini ukiwa na mwenzako unaweza *KUFURAHIA.* 

3. Ukiwa peke yako unaweza *KUTABASAMU,* lakini ukiwa na mwenzako mnaweza *KUCHEKA.*

Huo ndio *UZURI* wa mahusiano yetu kama binadamu. Tunategemeana. 

Kiwembe kina ukali lakini hakiwezi kukata mti; shoka lina nguvu na imara lakini haliwezi kukata nywele.

*Kila mtu ni muhimu kulingana na kusudio na lengo la uwepo wake. Usimdharau mtu yeyote kwa hali yoyote, kwa sababu huwezi kuwa yeye.*

*Mwenyezi Mungu atujaalie nguvu na moyo wa kusamehe, kustahmiliana na kuishi kwa upendo na umoja.*

Jumamosi, 26 Oktoba 2019

FAHAMU UWEZO WA NDEGE MPYA YA ATCL (Boeing 787 Dreemliner) KUTOKA NCHINI MAREKANI

Kwa kifupi ndege hii mpya iliyowasili Leo ina uwezo ufuatao

1*Ina uwezo wa kubeba jumla ya abiria 262
2*Ndege hiyo pia ina uwezo wa kubeba uzito wa tani 227. Uzito huo unajumuisha chombo, mizigo na mafuta. Sifa yake ni kwamba ina uwezo wa kuhimili hali nzito ya hewa ikiwa kwenye umbali mrefu kwenda juu.
3*Inabeba Lita 101,000 za mafuta na ukubwa wa mita 56.72 sawa na nusu ya uwanja wa mpira wa miguu.
Vilvile ndege hiyo ina uwezo wa kutembea kilomita 13620 sawa na saa zaidi 12 hewani bila ya kusimama

Alhamisi, 17 Oktoba 2019

HOW TO SUCCEEDED IN LIFE (Quote)

Infuse your life with action. Don't wait for it to happen. Make it happen. Make your own future. Make your own hope. Make your own love. And whatever your beliefs, honor your creator, not by passively waiting for grace to come down from upon high, but by doing what you can to make grace happen... yourself, right now, right down here on Earth

MAMBO MATANO YANAYOWEZA KUFUPISHA MAISHA YAKO, (Kusababisha uishi umri mfupi)

       Kwa kawaida maisha ya kibinadamu mwisho wake huwa ni kufa, hivyo kila mwenye pumzi hii leo mwisho wa maisha yake huishia kaburini.
Hata hivyo, kumekuwepo na viashiria fulani fulani ambavyo huweza kuashiria baadhi ya makundi fulani ya watu huenda wanaweza kuwa na muda mfupi wa kuishi duniani kutokana na sababu tofauti tofauti.
Miongoni mwa dalili ambazo huweza kuashiria mhusika anaweza kuwa na maisha mafupi duniani ni pamoja na hizi zifuatazo.

       1. Watu wenye kupenda maisha ya anasa na starehe
Watu wa aina hii huwa katika hatari ya kupoteza maisha haraka hata kabla ya siku zao kutokana na kuwa na hatari kubwa ya kupatwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo ya zinaa.

       2. Wavutaji wa sigara.
Watu wanaovuta sigara huwa katika hatari ya kuishi maisha mafupi zaidi kuliko wale ambao hawatumii sigara kwani watu wa aina hii huwa katika hatari ya kukumbwa na saratani ambayo huweza kukatisha uhai wa mhusika hata kabla ya siku zake.

       3. Kushinda umekaa siku nzima
Wale ambao huwa miili yao haina mazoezi kabisa nao huwa katika hatari ya kupoteza maisha mapema kutokana na kushambuliwa na magonjwa yasiyoambukiza kama vile shinikizo la damu, kisukari nk.
     
       4. Unywaji wa pombe
Watumiaji wa vileo na huwa katika hatari ya kupoteza maisha yao mapema kutokana na mambo mawili makuu
a) Kupata ajali kutokana na kutumia vyombo vya moto wakati wakiwa wamelewa na baadaye kujikuta wanapoteza maisha.
b) Ugomvi ambao huweza kuibuka kutokana na mihemko ya vilevi wanavyokuwa wamekunywa na kuweza kusababisha ugomvi mkubwa. Mfano kupigana na chupa na baadaye kupoteza uhai.

        5. Ulaji wa vyakula vya viwandani
Kuna wale ambao mara nyingi wamekuwa wakila vyakula vya makopo ambavyo vinapotumiwa mara kwa kwa mara huweza kuwa na madhara kadhaa likiwemo tatizo la saratani. Hivyo kundi hili nalo linaweza kuwa katika hatari ya kupoteza maisha kabla ya siku zao

Jumanne, 15 Oktoba 2019

MAJINA YA WANAFUNZI KUMI BORA WALIOFAULU MTIHANI WA DARASA LA SABA 2019

Hawa ndio wanafunzi vinara katika matokao ya mtihani wa darasa La saba mwaka 2019, kwa matokeo zaidi bofya link hapo,

https://results.necta.go.tz/results/2019/psle/psle.htm


Matokeo haya yametoka tarehe 15/10/2019 na kanda ya ziwa waibuka kuwa na matokeo mazuri zaidi,