Jumanne, 27 Septemba 2016

SHUGHULI UNAZOWEZA KUFANYA ILI KUJIONGEZEA KIPATO NJE YA AJIRA

      Niwasalimuni nyote na kuwashukuru kwa kufuatilia makala zangu.
       Leo napenda niwashirikishe juu ya "Shuguli unazoweza kufanya ili kujiongezea kipato nje ya ajira" Licha ya wasomi wengi kupenda kuajiriwa kuna changamoto nyingi zinazowafanya kuwa na kitu kingine cha kuwaongezea kipato. Hivyo siyo lazima uache Kazi ndipo uanzishe biashara, unaweza kuanzisha ukiwa kazini.
       Kama ilivyo ada siyo biashara zote unaweza kuzifanya ukiwa kazini hivyo zifuatazo in biashara tatu unazoweza kufanya ukiwa kazini na zikakuongezea kipato:-

    BIASHARA KWA NJIA YA  
                   MTANDAO.
     Unaweza kufanya hii biashara hata kama umeajiriwa.Unaweza kutangaza bidhaa unazoziuza na ukawa na siku maalum ya kufungua na kukutana na wateja wako walioweka oda ya bidhaa walizoziona mtandaoni.
     Hivyo kwa mwezi au wiki unaweza kugawa Siku unazopumzika na kuzitumia kuandaa na kuuza bidhaa zako.

    TUMIA KIPAJI ULICHONACHO
      Suala hili la kipaji nimelizungumzia kwa undani katika makala yangu inayosema KIPAJI CHAKO NI UTAJIRI TOSHA KATIKA MAISHA YAKO
  Unaweza kutumia kipaji chako kuwafundisha wengine na kuwapa ujuzi kwa njia ya malipo.
   Mfano; unajua kupika,kuimba,kuigiza,kughan nashairi au shughuli za ujasiriamali unaweza kutumia ujuzi huo kuanzisha kikundi cha mafunzo na kuingiza kipato kwa ule muda wako wa ziada.
      Hakikisha unajifunza  hata kwa kusoma mitandaoni jinsi wenzako wanavyofanya hicho kitu unachotaka kukifanya kabla ya kuanza ili uwe na ujuzi utakaovutia wengi kujifunza kutoka kwako.

     USHAURI NA HUDUMA ZA
                 KITAALAMU
      Kazi hii unaweza kufanya hatakama umeajiriwa, kwamfano ukiwa mhasibu unaweza kuwa na wateja nje ya Kazi ambao unakwenda kuwapigia hesabu zao, hiiinahitaji muda hivyo utajipanga kulingana na msimu, kama wewe ni mwalimu unaweza kutumia muda wa ziada kufundisha wanafunzi nyumbani kwako au kuwatembelea majumbani na kujiongezea kipato cha ziada.
    Naamini hadi kufikia hapo umejifunza jambo kamwe usiache kupitia blog yako pendwa ya innopri.blogspot.com upate maarufa zaidi.

Imeandaliwa na Innocent Prisckus,Kalunde Jamal kwa ushirikiano mkubwa wa MWANANCHI MEDIA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni