Jumatano, 23 Novemba 2016

MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUOA

*Nawaandikia ninyi vijana wa kiume na wanaume wote, maana mna nguvu na mmejaliwa na mwenyezi Mungu utashi, hekima na busara ili muweze kutawala kila kitu tokea kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu huu*.
```
1. Oa mwanamke ambae unaweza KUSALI nae na sio kwa sababu anajua MAPENZI vema.

2. Mwanaume bora KAMWE hapimwi kwa idadi ya wanawake alionao au aliotembea nao BALI kwa idadi ya wanawake aliowaambia "Mimi ni mume wa mtu" au ninae mtu tayari.

3. Kuna aina ya wanawake unatakiwa kuwaepuka kabisa kwa gharama yoyote ile, "wanawake wamaodhani uzuri wao ndio bora zaidi kuliko tabia zao"

4. Kila mwanamke anavutia akivaa nguo fupi inayoonesha maungo yake wazi, ila kama utakuta mwanamke amevaa nguo ndefu au za kusitiri mwili wake na bado anavutia, huyu ni dhahabu! Anathamini mali za mumewe!

5. Kamwe usimpe mwanamke mimba ya mtoto kabla hujampa mimba ya malengo na ukayatimiza.

6. Tafuta mwanamke ambae atakupa challenge ya maisha na kuongeza uwezo wako wa kufikiri na sio mwanamke wa kila kitu Ndio!

7. Wanawake wakamilifu hawapatikani popote duniani, ila wanawake bora wapo kila mahali.

8. Mwanamke anaweza kukusaliti, ila Mungu hawezi kukusaliti, hivyo basi kabla hujapata mwanamke Mpate Mungu kwanza. Kuna raha sana kuwa ndani ya Mungu asikwambie mtu!

9. Kama unajijua umefikisha miaka 25 na kuendelea epuka mambo ya kivulana, kuvaa suruali katikati ya makalio, kuvaa hereni, kubadili badili wanawake kama unachambua mitumba ya memorial

10. Usitumie kichwa chako kunyoa kiduku, tumia kichwa chako kuwaza mambo yenye tija ikiwemo kutafuta pesa na kuongeza hazina ya maarifa. ```

_*"Being a male is a matter of birth, being a man is a matter of age, but being a gentleman is a matter of choice. A best choice indeed!"*_

SABABU KUMI ZINAZOKUFANYA USHINDWE KUWA NA AKIBA

TABIA MBAYA KUMI ZINAZOFANYA USHINDWE KUWA NA AKIBA "SAVINGS"....HATIMAE UNAKOSA MTAJI WA KUFANYA MAMBO YAKO...

1.Unanunua nguo bila mpangilio..

Kuna watu wana nguo kama duka. Plz Kuwa na nguo chache Tu huwezi kushindana na fashion.

2.Unanunua Viatu bila mpango.

Viatu pia vinameza savings zetu. Nunua pea chache zenye ubora ili zidumu.

3.Unatoa ofa bar bila mpango.

Nenda bar kwa bajeti mahususi. Hakuna atakae kusifia kwa kutoa ofa hovyo. Kila mbuzi ale kwa urefu Wa kamba yake. Jifunze ubepari.

4.Unatumia hela nyingi kwenye simu ambazo sio productive. Unaweka vifurushi vya week vya sh 7000 au 10000 ili uchati na marafiki Fb au wasaap Huo ni ujinga. Badilika.

5.Unakopa hela benki na kununua vitu kama simu ya milioni na gari ambazo sio productive. Unakosa hela hata ya mafuta, gari la nini kwanini usingewekeza sehemu ili kuwe na mradi Wa kuzalisha ndio ununue gari?

6.Una marafiki wengi ambao ni mizigo kwako au hamuendani kivipato hivyo unajikuta unalazimika kutumia zaidi ya kipato chako ili uwa-impress. Meneja Wa TRA na mwalimu Wa sec unatarajia utoe offer mpaka umfurahishe meneja? Utabaki na sh ngapi toka kwenye salary yako?? Zinduka.

7.Huna timetable ya kudumu ya maisha yako, unajikuta unaburuzwa Tu na marafiki zako kwa kwenda sehemu mbalimbali za matumizi.

Kuwa na ratiba za maisha yako na zisimamie kikamilifu, usiburuzwe!

8.Una michepuko inayokutegemea wewe kwa kila kitu. Wanakuita ATM we we unakenua Tu huzinduki. Badilika.

9.Una huruma sana kuliko kipato chako. Yaani kila ukiombwa unatoa hata kama muombaji hana genuine need. Usiwe mkristo kuliko Yesu. Fanya hivyo kama ni lazima. Ila sio kila anaekupiga mzinga unapigika.

10.Unatembea na hela nyingi kwenye wallet au mshahara wote kwenye wallet au handbag au nyumbani kwako. Unapokuwa na petty cash nyingi unatengeneza mazingira ya kutumia hovyo. Jifunze kuweka hela benki. Tembea na hela Tu unayoihitaji kwa matumizi ya lazima.

Naamini tukizingatia kanuni hizi kumi tutaongeza savings zetu na kuwa na mtaji Wa kufanya vitu vikubwa endelevu.

Jumatatu, 31 Oktoba 2016

MAGONJWA YA KUKU NA TIBA ZAKE.

🐓🐓🐓🐓
UTANGULIZI
   Kuku kama wanyama wengine hushambuliwa na magonjwa mbalimbali ambayo mengine yanatibika kwa dawa na mengine hayana tiba bali kuku hupewa chanjo maalumu ambayo huzuia magonjwa hayo.Leo nitawaeleza baadhi ya magonjwa ambayo hushambulia kuku mara kwa mara na ambayo ni chanzo cha kuwakatisha tamaa wafugaji wa kuku.

A.) MAGONJWA YANAYOHITAJI CHANJO
     1> GUMBORO
                Ugonjwa huu husababishwa na virusi.
     
      DALILI ZA UGONJWA
    -Kuku kuzubaa na kulundikana, pamoja na kusinzia
    -Kuku kuharisha
    -Kuwa na vifo vingi kwa kuku

     TIBA
Ugonjwa huu hauna tiba,,Kuku wakipewa Dawa za oxytetracycline hupunguza vifo.

    KINGA
wakinge kuku wapo kwa kuwapa chanjo ya gumboro (Gumboro vaccine)

   2> MAHEPE (Marecks)
             Ugonjwa huu husababishwa na virusi

        DALILI
     -Kuku hupata ulemavu na vifo vya mara kwa mara.
  
    TIBA
Ugonjwa huu hauna tiba

    KINGA
Chanjo hutolewa kwa vifaranga wenye umri wa siku moja,vifaranga hupewa chanjo ya mahepe (Marecks vaccine)

   3>NDUI YA KUKU (Fowl Pox)
            Ugonjwa huu husababishwa na virusi.

     DALILI
    -Kuku hupatwa na vidonda kichwani.
    -Kuku hupata uvimbe mweupe kwenye mdomo na kushindwa kula.

      TIBA
Ugonjwa huu hauna tiba.

   KINGA
Chanja kuku wako wa siku 60-90 kwa chanjo ya Ndui ya kuku (Fowl pox vaccine).

  4>MDONDO (New castle)
           Ugonjwa huu husababishwa na virusi
 
   DALILI
  -Ugonjwa huu hutokea kwa ghafla na kuenea kwa haraka
  -Vifo vya kuku huwa vingi
  -kuku hupumua kwa  shida
  -Kuku hupooza na kulemaa miguu
  -Kuku hupinda shingo yake
  -Kuku hupunguza kutaga mayai
  -kuku huarisha
  -Kuku Kuzunguka zunguka na kutembea kinyume nyume.

   TIBA
Hauna tiba

    KINGA
  Chanja vifaranga wako na kuku wako kwa chanjo ya Mdondo (New castle vaccine) na urudie chanjo hii kila baada ya miezi mitatu.

B.)MAGONJWA YANAYOTIBIKA KWA DAWA

    1>KUHARA DAMU (coccidiosis)(Koksidiosisi
             Ugonjwa huu husababishwa na virusi.

    DALILI
-Kuku huzubaa na kujikunyata
-Kuku kuharisha kinyesi chenye damu au kinyesi cha kahawia
-Kuku hudhoofika,manyoya huvurugika na kulegea mabawa na kuonekana kama wawevaa koti
-Kuku hupungukiwa homa ya kula
-Vifo huwa vingi kwa vifaranga

TIBA
Wape kuku wako dawa kama Esb 3, Amprolium, au Basulfa.

KINGA
Zingatia usafi wa banda la kuku na usiruhusu unyevuunyevu katika banda la kuku,

   2>HOMA YA MATUMBO(Fowl typhoid)
        Husababishwa na bakteria

   DALILI
   -Kuku hupata homa kali
   -Kuku huarisha kinyesi cha kijani au njano
   -Vifo huwa vingi hasa kwa vifaranga wenye wiki 1-2
   -Kuku huzubaa,kuvimba viungo vya miguu,kuchechemea,kukosa hamu ya kula
   -Kuku wanaotaga hupunguza utagaji,hutaga mayai yenye ganda laini na hupata vifo vya ghafla

  TIBA
  Dawa za oxytetracycline kama Furamax,Typhoprim hutibu ugonjwa huu.

KINGA
  Hakikisha usafi wa banda na vyombo vya chakula na maji kwa kuku.
  Tenganisha kuku wagonjwa na wazima

C)MINYOO
Hushambulia kuku wote wakubwa na vifaranga

DALILI
-Kuku hukonda
-Kuku huarisha
-Kuku hukohoa
-Kuku hupunguza utagaji
-Kuku hudumaa katika ukuaji/hawakui vizuri
-Kuku hupungua uzito

TIBA
Tumia dawa za minyoo kama piperazine

KINGA
Wapewe dawa za minyoo mara kwa mara kila baada ya miezi mitatu

D)VIROBOTO/CHAWA/UTITIRI
   Hushambulia sana vifaranga na hutokea vifo kwa wingi kwa vifaranga Kwa kuku wakubwa tatizo halionekani kwa sana lakini nao huathiriwa sana.

DALILI
-Kuku kutochangamka
-Ukuaji mdogo wa kuku
-Kuku kutotaga na kuhatamia vizuri kutokana na kusumbuliwa na chawa,utitiri au  viroboto
-Viroboto huonekana kuganda machoni wakinyonya damu

TIBA
Tumia dawa za unga kama sevin dust 5% ,Malathion ,akheri powder kwa kuku wote na mabanda yao.

KINGA
Boresha usafi wa mabanda ya kuku.

E)UKOSEFU WA VITAMINI A
    huathiri sana kuku wadogo.

DALILI
   -Kuku huvimba macho na kutoa uchafu mzito kama  sabuni ya kipande iliyolowana.
   -Mara nyingi  ugonjwa hujitokeza baada ya kipindi kirefu cha kiangazi

TIBA
wape kuku wote dawa za vitamini.

Jumatano, 26 Oktoba 2016

HIZI NDIZO SIFA ZA MWANAMKE WA KUOA

   Wanaume wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba wanakurupuka tu na kuoa mwanamke yeyote mwenye sura nzuri, bali huchukua muda wao mwingi kuchunguza mambo mengi juu ya wake ambao wanadhani kwamba wanaweza kuwa pamoja kwa kipindi chote cha maisha.
     Wanawake wengi wanajisahau na kudhani kwamba kitu kinachowezakuwafanya wakapata wachumba niuzuri hivyo kupoteza muda wao kujichubua na kujiremba ili wawavutie wanaume bila kujua kwamba kuolewa ni zaidi ya uzuri.
     Hali sasa hivi imebadilika ni tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ukiwa na sura nzuri na umbo la kuvutia basi una asilimia 100 za kuolewa.
Utafiti ambao nimeufanya unaonesha kwamba zaidi ya uzuri wa tabia na umbo, kuna kuna sifa nyingine za msingi ambazo mwanamke anatakiwa kuwa nazo ili aweze kuwa katika mazingira mazuri ya kupata mchumba wa kumuoa kiasi kwamba asipokuwa nazo ataishia kuchezewa tu lakini haitatokea mtu kumtakiwa kwamba anataka kumuoa.

1. MWEYE MAPENZI YA KWELI
Lengo kubwa la mwanaume kuoa ni kutaka kupata mapenzi ya kweli kutoka kwa mwanamke na ikiwezekana waweze kupata watotoa ambapo watoto mara ndio wamekuwa furaha ya ndoa. Wapo wanawake wengine ambao wanonesha wazi kutokuwa na mapenzi ya kweli bali wanakuwa na mapenzi ya kuzuga. Wanachotaka wao aidha kupata umaarufu tu kwamba yuko na mtu fulani ama kuweza kupata pesa alizonazo mwanaume lakini sio kwamba ana mapenzi ya dhati kutoka moyoni mwake.
Mwanamke asiye na mapenzi ya dhati utamgundua tu, muda mwingiutamuona macho yake yako kwenye mfuko wa mwanaume. Akiona kwamba mfuko umetuna utaona anaonesha mapenzi ya hali ya juu lakini pindi hali inapokuwa kubwa mbaya kifedha mapenzi yanaanza kufifia.
Kwanini wanaume wanapenda wana wake wenye mapenzi ya dhati kutoka mioyoni mwao na si kutokana na fedha walizonazo? Hii inatokana na ukweli kwamba maisha siku zote yanabadilika, kama waswahili wanavyosema, kuna kupanda na kushuka.
Sio kwamba kila siku utakuwa na maisha mazuri na kama itatokea hivyo basi ushukuru mungu.Hivyo basi mwanamke wa kuoa lazima afahamu hivyo na awe tayari kuonesha mapenzi yake ya dhati wakati wote wa maisha yao na si kwa kipindi fulani tu cha neema.
Si hivyo tu pia asilimia kubwa ya maisha ya ndoa yanatawaliwa na mapenzi, kwa hiyo nyanja hiyo inakuwa ya msingi sana kwa wanaume wengi kuiangalia ili wasije wakajikuta wanaoa mwanamke ambaye baada ya muda mapenzi yanakwenda likizo hali ambayo inaweza kuwafanya wasiishi maisha ya raha mustarehe.

2. WENYE TABIA NZURI
Tabia njema ndio silaha ya maisha, ukiwa na tabia nzuri kila mtu atakupenda, hiyo ni katika maisha ya kawaida. Lakini linapokuja sualana kuoa tabia inakuwa kitu cha awali sana kungaliwa na hiyo inaweza kuwa na ukweli kwa sababu wapo wasichana wazuri wenye mvuto wa aina yake na maumbile mazuri, lakini wanakosa wanaume wa kuwaoa, ukiuliza kwani utaambiwa anatabia mbaya.
Naweza kusema hilo ndilo limekuwa tatizo kubwa kwa baadhi ya wanawake kukosa wanaume wa kuwaona. Hakuna mwanaume hata mmoja kati ya wale ambao nimejaribu kuongea naye ambaye ameonesha kulidharau suala hilo la tabia.
Si hivyo tu wapo wanaume ambao wameingia kichwa kichwa na kuoa kwa kuangalia sura tu bila kujali tabia, matokeo yake baada ya siku chache yanatokea machafuko ya aina yake hali ambayo imepelekea kuvunjika kwa ndoa kutokana na tabia mbaya alizonazo mwanamke.

3. WENYE UCHU NA MAENDELEO
Hivi karibuni kumekuwepo na mabadiliko ya aina yake kwa wanaume, wengi sasa hivi hawapendi kabisa kuoa mwanamke ambaye hana kazi yaani ‘golikipa’. Kama atakuwa hana kazi basi awe na uchu wa maendeleo kwa kujituma kufanya kazi mbalimbali za kimaendeleo kama vile kilimo kwa wale walio vijijini na biashara ndogondogo kwa wale ambao wako mijijini na hata vijijini.
Ile dhana ya kusema mwanamke ni mama wa nyumbani wa kukaa na kujipodoa akimsubiria mwnaume arudi amstarehesha, sasa hivi imepitwa na wakati. Wanaume wengi wanapenda wanawake ambao ni wahangaikaji, wenye ndoto za maendeleo katika maisha yao. Hata kama watakuwa si wafanyakazi lakini wawe wenye kutoa ushauri kwa waume zao juu ya jinsi gani wafanye ili wafanikiwe.

    4. WASIOPENDA MAKUU
Kuna wanawake wengine wanakuwa na tabia za ajabu sana kiasi kwamba yaweza kuwa kero kwa wanaume. Wapo wanawake ambao wanapenda makuu bila kujali hali halisi ilivyo. Kuna wanawake naweza kusema wana tamaa, kila wikiendi utamsikia “leo tunakwenda wapi dear?”
Akimuona rafiki yake kanunua simuya laki tatu na yeye utamsikia akisema, ‘na mimi naomba uninunulie simu kama ya Grace’. Ukienda naye Pub anakuambia,”mimi sinywi pombe za chupa natumia za kopo tena Heineken’. Yeye hajali kiasi cha pesa mwanaume alicho nacho na usipotekelezea anachukia na anaweza hata kupunguza mapenzi.
Wanawake kama hawa wako katika mazingira magumu sana ya kuweza kupata wanaume wa kuwaoa. Mara nyingi katika maisha fedha huzungumza, kama mwanaume atakuwa na pesa ya kutosha itakuwa rahisi sana kwa mwanamke kupata kila atakachopenda lakini si kwa kumwambia mimi nataka kitu fulani.Mwanaune mwenyewe utamsikia akisema, ‘unataka nikununulie simu ya aina gani, au leo unataka twende wapi?’ hapo ndipo utakuwa na nafasi ya kusema, ‘mimi nataka uninunulie simu kama ya fulani ama leo nataka twende sehemu fulani.’
Wanaume ni warahisi sana wa kuwapatia wale ambao wanatarajia kuwaoa chochote ambacho watahitaji kama tu pesa haitakuwa tatizo. Kitu ambacho kinawaudhi wanaume wengi ni ile tabia ya mwanamke kupenda mambo makubwa bila kuangalia uwezo uliopo kwa mwanume.
Kuna wanawake wengine wao si wasemaji kabisa, yeye anasubiri leoamemletea hiki, anapokea na kushukuru, kesho akiambiwa twende beach anakubali. Au wengine wanasubiri mpaka waulizwe wanataka nini, ndio wanasema.
Sisemi kwamba uwe mkimya tu hata kama una shida ya kitu fulani na unafahamu kwamba ukimweleza mwenza wako anaweza kukusaidia, hapana! kama unaona kwamba uwezekano wa kupata kile ambacho unakihitajiupo mweleze kwa utaratibu naamini atakuelewa na kukutimizia.Tabia ambayo hawaipendi wanaume wengi ni ile ya kulazimisha ufanyiwe kitu fulaniwakati inawezekana uwezekano haupo.

         5. WAVUMILIVU
Wapo wanawake ambao sio wavumilivu kabisa katika maisha.Tunajua kwamba maisha siku zote hayatabiriki, yanaweza kutokea matatizo ya kiafya ama kifedha.Huu ndio wakati wa kuona uvumilivu wa mtu.Kama mwanamke anatarajia kwamba siku zote ni za raha tu na pindi matatizo yanapotokea anachukua uamuzi wa kumtoroka mwanume, huyo siyo mwanamke wa kuoa.
Wangapi leo hii huwatoroka waume zao pindi inapotokea kuumwa, kufilisika ama kupatwa na tatizo lolote ambalo kwa namna moja ama nyingine yanaweza kuwafanya maisha yao kutingishika?
Uvumilivu kwa mwanamke utakuwepo kama tu atakuwa na mapenzi ya dhati kama nilivyozungumza hapo awali. Mwanamke mweye mapenzi ya dhati ni lazima atakuwa mvumilivu na atakuwa tayari kuishi katika maisha ya aina yoyote, yawe ya raha ama ya starehe.Hawa ndio wale ambao wanaume wengi wengependa kuwa nao maishani mwao.
Licha ya kupenda kuoa wanawake amabo wana tabia hizo nilizozitaja hapo juu, wanachukizwa sana na wanawake ambao wanavijitabia vidogo vidogo ambavyo kimsingi havikubaliki katka jamii.
Tabia hizo ni kama wambea, wasio wakweli na wawazi, wasioridhika, wagumu kusamehe na wapesi wa kuchukia, wagomvi na wenye roho ya kwanini.
Utafiti huu umefanyikwa kwa baadhi ya wanaume ambao wanatarajia kuoa wanawake ambao wanaoishi katika maeneo mbalimbali
Kwa maana hiyo basi hiyo iwe changamoto kwa wanawake. Wajue kwamba wanaume wanafurahi kuwa na wanawake wa aina gani. Hata kama utakuwa umeshaolewa, kama kuna wakati kunakuwa na kutokuelewana baina yenu, chunguza yawezekana kwamba unakosa mojawapo ya tabia ambazo nimezitaja hapo juu. Waweza kubadilika kwani inawezekana.

Jumanne, 27 Septemba 2016

SHUGHULI UNAZOWEZA KUFANYA ILI KUJIONGEZEA KIPATO NJE YA AJIRA

      Niwasalimuni nyote na kuwashukuru kwa kufuatilia makala zangu.
       Leo napenda niwashirikishe juu ya "Shuguli unazoweza kufanya ili kujiongezea kipato nje ya ajira" Licha ya wasomi wengi kupenda kuajiriwa kuna changamoto nyingi zinazowafanya kuwa na kitu kingine cha kuwaongezea kipato. Hivyo siyo lazima uache Kazi ndipo uanzishe biashara, unaweza kuanzisha ukiwa kazini.
       Kama ilivyo ada siyo biashara zote unaweza kuzifanya ukiwa kazini hivyo zifuatazo in biashara tatu unazoweza kufanya ukiwa kazini na zikakuongezea kipato:-

    BIASHARA KWA NJIA YA  
                   MTANDAO.
     Unaweza kufanya hii biashara hata kama umeajiriwa.Unaweza kutangaza bidhaa unazoziuza na ukawa na siku maalum ya kufungua na kukutana na wateja wako walioweka oda ya bidhaa walizoziona mtandaoni.
     Hivyo kwa mwezi au wiki unaweza kugawa Siku unazopumzika na kuzitumia kuandaa na kuuza bidhaa zako.

    TUMIA KIPAJI ULICHONACHO
      Suala hili la kipaji nimelizungumzia kwa undani katika makala yangu inayosema KIPAJI CHAKO NI UTAJIRI TOSHA KATIKA MAISHA YAKO
  Unaweza kutumia kipaji chako kuwafundisha wengine na kuwapa ujuzi kwa njia ya malipo.
   Mfano; unajua kupika,kuimba,kuigiza,kughan nashairi au shughuli za ujasiriamali unaweza kutumia ujuzi huo kuanzisha kikundi cha mafunzo na kuingiza kipato kwa ule muda wako wa ziada.
      Hakikisha unajifunza  hata kwa kusoma mitandaoni jinsi wenzako wanavyofanya hicho kitu unachotaka kukifanya kabla ya kuanza ili uwe na ujuzi utakaovutia wengi kujifunza kutoka kwako.

     USHAURI NA HUDUMA ZA
                 KITAALAMU
      Kazi hii unaweza kufanya hatakama umeajiriwa, kwamfano ukiwa mhasibu unaweza kuwa na wateja nje ya Kazi ambao unakwenda kuwapigia hesabu zao, hiiinahitaji muda hivyo utajipanga kulingana na msimu, kama wewe ni mwalimu unaweza kutumia muda wa ziada kufundisha wanafunzi nyumbani kwako au kuwatembelea majumbani na kujiongezea kipato cha ziada.
    Naamini hadi kufikia hapo umejifunza jambo kamwe usiache kupitia blog yako pendwa ya innopri.blogspot.com upate maarufa zaidi.

Imeandaliwa na Innocent Prisckus,Kalunde Jamal kwa ushirikiano mkubwa wa MWANANCHI MEDIA.

Alhamisi, 25 Agosti 2016

MAISHA NI MIAKA 40 TUU SOMA HAPA UJIFUNZE.

.
*LIFE BEGINS AT 40.... HOW OLD ARE YOU?*

Life Begins at 40..

Huo ni msemo wanao waingereza wakimaanisha maisha yako ijapokuwa yanaanza toka milele iliyopita na toka umeumbwa au toka umefika duniani na toka umeanza kukua nk nk lakini bana maisha #halisi yataanza rasmi siku ukitimiza miaka 40.

Hapo kama bado nauli ya daladala ni ishu, ada, chakula, kodi ya nyumba, nk basi ndo utaanza kuelewa maana ya muda uliokuwa unatumia Facebook kulike picha za ajabu na story zisizokupeleka popote.
Nadhani unanielewa sasa hasa wewe ambaye unahisi umri wako bado ni mdogo kwa hiyo bado bado kidogo muda wa kuwa serious na maisha haujafika.
Sikia kijana mwenzangu..TODAY is your future kwa taarifa yako.. Ulipokuwa mdogo ulisema nikiwa mkubwa nitakuwa na gari na nyumba nzuri wazazi wangu wataishi hivi na vile. Je unayo? Je imetokea? Maybe yes. But maybe no.

Kama haijatokea je bado hujawa mkubwa? Basi kama ni mkubwa ujue kuna kitu hujafanya.

Utasema tena nikifika miaka 40 nataka niwe na hiki na kile watoto wangu wasome international school nk. Subiri uone miaka inavyoenda. Usishangae kufika 40 bado umeajiriwa kwa mtu na anakugombeza kwa nini mwanao anaumwa kila siku unachelewa kazini. Kazi nyingi. No bright future. No enjoyable present. Just existing and not living!

Hapo ndo unawaza kufuga ng'ombe wa maziwa Kibamba kwenye kiwanja chako cha miguu 12 kwa 15! Wenzako wa umri wako hapo unasikia wameanzisha bizness in Australia. Wamenunua kiwanja Mbezi Beach kwa 300M! Wamejenga mjengo wa ukweli. Wanamiliki Apartment Johannesburg. Wakienda UK wanaenda kula The Ritz (Google that). Wanasomesha watoto zao the finest schools available wewe wa kwako wakati huo wamekosa nafasi Makongo wameenda Kibamba Secondary School wanapanda daladala sita kwenda na kurudi full kutukanwa na makondakta.

Wenzako in their 40s wanasaidia wasio na uwezo katika jamii wewe ndo kwanza ukipokea simu kutoka kijijini mzazi anahitaji support kidogo una-mute! Wenzako in their 40s wakisikia kuna ujenzi wa nyumba ya ibada wanachangia 5M kimyakimya.. Wewe ukitoa laki moja basi mpaka mtaa wa saba watajua! Halafu unashangaa wenzako wanazidi kuinuliwa. Unaanza kuwaita Freemason.  Mwenye nacho ataongezewa au hujui? Na asiye nacho..... (Malizia). Wakati wenzako walikuwa wanajenga maisha wewe ulikuwa unashinda Facebook kuongelea UKUTA uwepo au usiwepo.. Harmonize anajua kuomba au hajui. Wema Sepetu atafute mtoto au aache tu. Can you imagine?

Wenzako mkifika miaka 40 watu wa rika lako wana exposure ya uhakika. Wewe at 40 bado umeajiriwa na mchana unakula kwa mama lishe chakula hata virutubisho hakina.  Wenzako at 40 washaacha ajira siku nyingi washatembea dunia na kujifunza maisha kutoka kila mahali. Walishafika kuanzia Sauzi, Botswana, Mozambique, Kenya, Ethiopia, Ghana, Naija, mpaka Egypt, The UK, Australia, Hawaii, Mexico, Croatia, The Netherlands, Switzerland, US, Panama mpaka Puerto Rico, Brazil na jirani zake, Hong Kong, Australia, Japan, China, (Incredible) India, Thailand, Singapore, New Zealand, Comorros, you name it..!! Wewe hata Kampala hujawahi fika. Kila siku Tegeta Posta ndo ruti yako miaka 15 mfululizo eti unatafutia watoto maisha! Unaishi au unaisha?

Acha mawazo mgando. Eti mi nina mshahara mzuri. Mshahara mzuri? Kweli?  Sikia, hiyo ajira ifanye serious sana tu lakini kwa muda tu. Jiandae kusimama mwenyewe. Kwani hujiamini? Na Mungu naye humwamini? Changamoto ni sehemu tu ya kufika kileleni. Don't be afraid. Don't dwell in that comfort zone!! Unasubiri kiinua mgongo? Utaenda kukiinvest wapi na kwa nguvu ipi. Na utaenjoy retirement kweli kama at 60 yrs ndo unafungua duka la vifaa vya ujenzi eti vinalipa. Kwa nini hukufungua ukiwa 30 ili uone vinalipa au la. At 60? With due respect.

Suffer the pain of discipline now. Or else you will suffer the pain of REGRET. Halafu ukianza kuregret ndo pressure zinakuja, stress, nk mwisho unawacha hata hao watoto in a far worse situation than your own lifetime. Kisa? Ulikuwa unatumia muda wote kuangalia vitu vya kuchekesha chekesha na kuongelea mambo ya siasa sijui wasanii sijui msanii gani ana hela nyingi sijui nani kafulia sijui nani ana mimba.. Seriously? Sijui nani hajapendeza kunyoa bora asuke😡😠😠.  Utashangaa umri unaenda bila kupiga hatua. Umri wako ni kila sekunde na kila dakika na kila saa.  Ndo umri huo.  Ndo maana matajiri wanalinda muda wao kwa wivu mkali. Coz TIME IS MONEY.  Utashangaa unafika 40 years ndo unawaza uanzie wapi. Mungu siyo mjinga kukupa umri huu wa ujana. Hajakupa uuchezee chezee tu. Be careful.  Time flies.

Life Begins at 40 my friend.. How Old Are You? So kama wewe unasema "Mimi bado mdogo.." endelea tu kupoteza muda wako utakumbuka tu siku moja but it might be too late. Endelea tu kupoteza muda na skendo za wasanii. Au unakuta mtu ameajiriwa au amejiajiri miaka inaenda hajui kwa nini hapigi hatua kipato hakikui lakini yupo tu hatafuti maarifa ya jinsi gani ya kutumia muda wake wa ziada kutengeneza kipato hata mara mbili ya mshahara wake. Wengine wanafanya hivyo na wanapiga hatua kubwa hadi wengine wanafikiria sasa kuachana na ajira. Ni muhimu kujifunza haya mambo. Siasa hazitaisha. Angalia your life. Ukifika 40 years uwe very established. Bila hivyo utashangaa kweli. Wakati wenzako wachache wa rika lako mtakapofika miaka 40 wakati wenzako unasikia amenunua kiwanja Kurasini kwa sh Bilioni mbili kwa ajili ya *kupaki* tu Masemitrela zake kama 20 hivi wewe wakati huo unashangaa Kama Kurasini kumbe kuna viwanja? Wakati huo wewe unamiliki kigari cha mkopo unakipaki uwanja wa CCM unalipia sh 1000/- tu, mnaita buku. Fikiria vitu kama hivi. Utajua vizuri umuhimu wa kutumia muda wako vizuri.  Ilikuwa January sasa September inabisha hodi. Mwaka unayotumia.  Wewe mwaka huu nini kipya hasa umefanya kimaendeleo. Usiseme nimepata ajira. Ajira haikupeleki popote. Njoo kwetu ujifunze vizuri.

+255757788444/+255672747666

Jumanne, 23 Agosti 2016

JINSI YA KUTUNZA FEDHA

       1.Kuwa na nidhamu ya pesa.
Watu wengi tumekua tukidharau fedha hasa zika ndogo, ni vizur kuheshim fedha hiyo na kuweka mikakati ya kuiongezea zaidi,

     2.Tumia pesa kwa malengo.
Wakati wa kutumia fedha hakikisha hutoi tuu Bali unakua na lengo maalum la kutoa fedha hiyo,
    Mara nyingi to a fedha itakayoenda kuzalisha kuliko kupoteza hela bure.

        3.Angalia matumizi yako unapokua na marafiki.
Mara nyingi huwa tunajisahau tunapokua na marafiki zetu sehemu za starehe almaarufu kama "Sehemu za bhatta" epuka kutumia fedha nyingi kutoa ofa maeneo kama haya.

       4.Fanya uwekezaji.
Unapowekeza fedha mahali Fulani ni vigumu kuitumia ovyo maana itakua katika mzunguko,
      Watanzania wengi tumejengewa fikra kuwa ili uwekeze lazima uwe na fedha nyingi kampuni au eneokubwa pamoja na wafanyakazi wengi, hii siyo kweli, unaweza ukawekeza hata kwenye kilimo,au,ufugaji Mdogo tuu na baadae ukafurahia uwekezaji wako.

      5.Andika nakala ya kila fedha utakayotumia.
Kuwepo na mpango wa mapato na matumizi ya fedha ulkila siku.
   Hapa tunaangalia matumizi madogomadogo ambayo wengi hawayaaandiki mfano, unaponunua Maji,soda,vocha,vtafunwa kma bablish,karanga na biscut huwa ni matumizi madogo lakini yanatumia fedha nyingi nje ya mipango yako ya siku,
   Pia ni vyema kuandika fedha itakayoingia kwa siku na kufunga hesabu kila mwezi, hapa utafahamu tofauti juu ya mapato yako na matumizi yako kwa mwezi

Kwa maelezo zaidi juu ya hayo tutafute hapa +25575778844/+255672747666.

Imeandaliwa na Innocent Priscus na msaada mkubwa kutoka kwa Vanilla Damma.