Jumatatu, 24 Agosti 2015

KUISHI KWA FURAHA SIKU ZOTE

>Katika maisha huwa tunakutana na mambo mengi ambayo kiukweli sio yote yatatupa furaha,,hii ni kutokana na tofauti zetu sisi wanadamu...

°Kama umeudhika na jambo fulan   cyo chanzo  cha kununa na kukosa raha chukulia poa na anza kutafuta suluhu ya tatizo hilo ili uc ufhike tena....
°Ishi maisha ya furaha Share love na watu wote utafanikiwa sana

NB:usizarau mawazo ya mwenzako hata kama anaongea ujinga 'tumia ujinga wake kujielimisha'

Imeandaliwa na kuletwa kwako na INNOCENT PRISCUS mobile 0767788444_

Jumamosi, 15 Agosti 2015

FAHAMU MISEMO MBALIMBALI YA KIKABILA YENYE NAANA KUBWA KATIKA MAISHA YAKO

1. Acha kukuna makovu ya mende(Kichaga)
Maana yake ni kwamba uache kukumbuka taabu ya wakati uliopita. Methali hii itafahamika vizuri kama tukielewa kwamba hapo zamani katika jamii zetu, mende walikuwa wanaonekana kwa wingi katika nyumba. Nao mende ni hodari wa kuuma watu wakati wa usiku wakiwa wamelala. Na pale walipouma hubaki kovu ambalo hukuna. Lakini pia ambaye ameshaumwa na mende hao itakuwa ni kazi bure kama atakalia kuyakuna makovu hayo.
Methali hii hutumika kwa kuwaonya watu wasikalie kufikiria makosa au taabu za wakati uliopita.

2. Afadhali kuchakaza nguo kuliko akili(Kipare)
Maana yake ni kuwa hakuna kitu bora kama akili (hekima). Mtu ambaye hana hekima ya uchi kuliko uchi wa aina yoyote ile. Kuwa uchi kinguo, mtu anaweza kununua zingine. Lakini mtu anapokuwa uchi kiakili, hakuna maarifa.
Methali hii hutumika kwa kumhurumia mtu ambaye ameharibikiwa na akili na anafanya majambo isivyotakiwa katika jamii.

3. Amekufa hata Mwakafwile aliacha mwana alipokufa (Kinyakyusa)
Methali hii inatokana na mila za kibantu kukosa mrithi ni mwisho wa ukoo na jina la ukoo. Mtoto wa kiume huendeleza ukoo. Ni jambo la kusikitisha sana kutokuwa na mwana mrithi.
Maana ya methali hii ni kwamba mtu anayehusika hana msaada wowote kutoka kwa ndugu, jirani au mahali penginepo.
Hutumika na mtu binafsi aliyezama ndani ya kilindi kikubwa cha matatizo, wala hana mtoto au mtu wa karibu naye ambaye angeweza kumsaidia. Ni methali ya watu maskini na wanyonge katika kuhurumiana shidani. Kama kuunguliwa nyumba, kufiwa nk.

4. Anayetaka usawa mwisho wake uchawi (Kikerewe)
Methali hii ina maana kwamba tukubali kuwa binadamu budi kutofautiana. Fulani kapata baiskeli – lazima nami nipate, fulani kapata nyumba – lazima nami nipate nk. Maneno kama haya mwishowe humsukuma mtu kutumia hila mbaya au njia zisizo za kawaida kama vile uchawi.
Methali hii hutumika katika kuwaonya wanopenda kujikweza.

5.Fimbo ya jirani haiui nyoka (Kiiraqw)
Ujirani ni jambo jema lakini si vizuri kutegemea misaada yote toka kwa majirani. Methali hii inafundisha umuhimu wa kujitegemea na si kutazamia kupata misaada kila uhitajipo.Pia, ni lazima ieleweke kwamba hakuna sheria inayomfanya jirani atoe msaada hata kama anaweza, yote hutegemea matakwa yake na huwezi kubashiri ni lini atakataa kutoa msaada.

6. Fungo alikosa mkia kwa kulala(Kizigua na kinguu)
Ipo hadithi katika hadithi za Kizigua na Kinguu isemayo kuwa kwa sababu ya usingizi wake Fungo alikosa au aliupoteza mkia wake. Methali hii inaonyesha hasara ya uzembe na kuchelewa mara nyingi. Hali hii inaweza kumkosesha mtu mambo mengi mazuri au kupoteza maslahi yake ambayo yangemfaa baadaye. Hutumika kama onyo kwa wazembe.

7. Anayelala na mgonjwa ndiye anayejua miugulio (Kisambaa)
Maana yake ni kwamba huwezi kujua undani wa mtu mpaka uwe naye karibu katika uhusiano. Hutumika kwa mtu anayejitia kujua sana mambo ya ndani ya wengine kuliko wenyewe wanaohusika.

8. Hohehahe hakosi siku yake (Kiha)
Maana yake ni kuwa kila mtu ana bahati yake. Hata maskini ana siku yake ya bahati. Hutumika kama onyo kuwa inafaa kuthamini watu kwa utu wao na wala si kwa mali walizonazo. Mtu ni utu.

9. Kondoo wa madoadoa hawako katika jamii ya wanadamu (Kimasai)
Wanadamu wote hawahitilafiani sana kwa maumbile yao, na ndio maana tunaweza kusema, binadamu wote ni sawa. Tusikiapo kitu kisicho cha kawaida kuhusu mtu tunaweza kutumia msemo huu kumaanisha kwamba tumestaajabishwa na habari hizo. Msemo huu unatumika pia katika kukanusha habari zisizoaminika.

10. Kucheka chongo ya mwenzio na hali yako umefunika (Kisukuma)
Maana yake ni kuwa si vizuri kucheka makosa ya wengine kwani huenda ukafanya makosa yale yale na pengine una udhaifu wako ambao wengine wanakucheka. Hutumika katika kuwaonya watu wanaocheka dosari au udhaifu wa watu wengine na pengine watu wanaocheka wenzao waliopatwa na maafa k.m. kufilisika.

11. Mbwa mwenye mnofu mdomoni hapigi kelele (Kifipa) Maana yake ni kama methali ya kiswahili isemayo:- Mwenye shibe hamjui mwenye njaa. Methali hii hutumiwa kwa kuwasema watu ambao wana kitu na huwasahau wale ambao hawana kitu. Zaidi, huweza kutumika kwa kuwaonya viongozi wanaosahau kuwatetea wenzao baada ya kupata madaraka na shibe.

12. Mwenda usiku amesifiwa kulipokucha (Kikwere) Mwenda usiku hapa ni sawa na mtu ayetenda jambo ambalo kwa wakati ule wengine hawalielewi. Lakini mwishowe jambo hilo lilipoonyesha mafanikio ndipo watu wakaanza kumsifu. Hutumika kwa mtu anayechekwa na wenziwe juu ya jambo alitendalo iwapo wakati ule wale wamchekeo hawaelewi usahihi wa lile alitendalo.

13. Nguo ya mzee haikosi chawa(kimeru) Maana yake, mzee hakosi akiba. Maana ya methali hii itafahamika zaidi si kwa vile hali ya uchafu ndiyo iletayo chawa, bali kwamba kwa mzee huwa na akiba za aina aina nayo maana yake ni ile nzuri. Methali hii hutumika wakati mtu anapozungumzia utajiri wa mtu mzee. Ni kama njia ya kuwakoga wengine kwamba wakati wote utazamie kumkuta mzee katka hali nzuri, anayo akiba yake ambayo ameihifadhi.

14. Usidharau wakunga uzazi ungalipo(Kibena) Wakunga ni watu wenye kuheshimiwa sana kwa sababu ya ufundi na ujuzi wao wakati wa kuzalisha. Kwa kuchukua umuhimu wao huo, wanawake hushauriwa kutowadharau maadamu wangali wanazaa, isijeikawa wakti wa kujifungua wakakosa msaada. Matumizi ya methali hii ni kuwaonya watu kwa ujumla wasiwe na dharau kwa kitu ambacho kitawafaa katika maisha yao. Zaidi kwamba, kitu kilichokusaidi wakati uliopita usikidharau kwa vile hukitumii kwa wakati huu.

Jumatatu, 10 Agosti 2015

JE WAJUA HILI? KUWA MAKINI.

Watu wote wamezaliwa huru, hadhi na haki zao ni sawa. Wote wamejaliwa akili na dhamiri, hivyo yapasa watendeane kindugu.

All human beings are born free and equal in dignity and rights. They are endowed with reason and conscience and should act towards one another in a spirit of brotherhood.

Jumapili, 9 Agosti 2015

JINSI NDOTO ZAKO ZINAVYOWEZA KUKUJENGEA MAFANIKIO MAKUBWA MAISHANI.

OTA NDOTO MPYA YA MAFANIKIO

IPE nafsi yako raha kwa kuota ndoto. Si ndoto yoyote bali ndoto ya kuwa na malengo makubwa.
Binafsi ninaamini katika malengo hayo kuwa kuna mafanikio endapo utamaanisha.
Wakati mtu anapoanza kuwa na malengo makubwa anaanza kwa kufikiri jinsi Mungu alivyomwezesha mtu kufikiri jambo hata kufikia uamuzi wa kuchukua hatua na kufanikiwa.
Mtu mmoja aliandika barua na kusema kuwa wana mpango wa kuwa na mashindano maalumu ya michezo.
Aliendelea kusema kuwa wamepanga kushinda mashindano ya kitaifa ya mpira wa kikapu, kama siyo mwaka huu itakuwa mwaka ujao, au vyoyote itakavyokuwa ili mradi wafikie lengo hilo.
Kocha wa timu hiyo alijua nia hiyo hivyo alikuwa akiwatia moyo wachezaji wake kwamba watashinda.
Mashindano hayo yalipofika kweli walishinda hivyo ndoto ya ushindi iliyokuwepo ilitimia.
Ndoto haina gharama. Kumbuka ukiwa na malengo ya mafanikio haitakugharimu chochote.
Unaweza ukawa na malengo ya kuanzisha mradi mkubwa pasipokuwa na fedha, inabakia kuwa ni ndoto tu.
Mungu alianza kuumba dunia ikiwa haina kitu. Tunaweza kuwa na malengo makubwa ya mafanikio katika maisha yetu haijalishi ni ya aina gani.
Endelea mbele ukiachia fikira zako kufikiri. Kama moyo wako umevunjika au upo katika hali ya kukata tamaa au umejaa wasiwasi, unatakiwa kuwa na ndoto mpya mapema iwezekanavyo.
Unapohitaji muujiza unatakiwa kuwa na maono mapya katika maisha yako.
Kumbuka hata wewe unaweza ukawa na maono makubwa ya ajabu. Haijalishi ni mtu wa aina gani, au umetoka wapi, au umepatwa na jambo gani?
Katika hali uliyonayo unaweza kuwa na maono mapya. Malengo makubwa si kwa wale waliofanikiwa, bali ni kwa wale wanaotaka kufanikiwa.
Inawezekana ukawa una fikra kama za mwanamke mmoja niliyekutana naye siku za karibuni ambaye alikuwa ameachwa na mumewe, ndoto yake ilikuwa ipo siku atakutana na mtu ambaye kwa pamoja watatengeneza na kujenga nyumba yenye upendo na mafanikio.
Vyovyote uwazavyo, ndoto inainua, inaweka kitu kipya katika maisha yetu, inatutengeneza na kutusogeza mbele, inatuwezesha kufikia malengo makubwa tofauti na ilivyokuwa awali.
Inatuwezesha kufanya kitu kikubwa ambacho hujawahi kukifanya tena kabla ya hapo.
Je, wataka kuwa fulani? Kusimama nje ya kusanyiko kubwa? Kukumbukwa? Hali hiyo inakuwepo ndani ya mioyo yetu inayodunda na kutaka kupata siri ya mafanikio.
Tunataka kuwa fulani. Inawezekana ndiyo inawezekana. Mungu ametoa kwa kila mtu uwezo na vipaji mbalimbali.
Wakati Mungu anakuumba alikupa kipaji na akasema kama utatumia kipaji ulichonacho atakiongeza, na kama hutatumia kipaji ulichonacho utakipoteza. Kukitumia kipaji chako au kukiachia ni juu yako wewe!
Dunia yetu imejaa vipaji vingi na uwezo ambao hautumiwi. Unatakiwa kulima kwa bidii, kupalilia ili upate mavuno bora. Tumia kipaji chako kabla hujakipoteza.
Unaweza kudhani kuwa hauna kipaji chochote si kweli labda inawezekana ujagundua kipaji chako. Inawezekana umekiweka kipaji chako kabatini. Amini kuwa kila mmoja anacho kipaji chake alichopewa na Mungu.
Waweza kutumia kipaji ulichonacho au kukipoteza. Maisha yetu yamejengwa katika kanuni hiyo. Kuna mifano mingi ya kupoteza au kupata hiyo ni kanuni ya kawaida.
Chukua hatua tano ambazo zitaifanya ndoto yako kuwa ya kweli.
Ota ndoto yenye thamani katika maisha yako. Kama hauna malengo, haitawezekana matarajio yako kutimia.
Ndoto inaanza unapokuwa na wazo. Kumbuka watu huvutiwa na wenye maono makubwa.
Chagua maono yale yenye matarajio. Baadhi ya watu wanapoteza muda wao kwa kuwa na malengo ambayo hayatawasaidia.
Mfano kuna kijana mmoja miaka iliyopita alisaidiwa kupewa ushauri baada ya kupoteza muda wake mwingi akifikiria ni jinsi gani ataweza kumpata mke wa jirani yake na kumfanya awe mke wake. Ndoto yake hiyo haikuwa ya thamani, ya muda mrefu.
Wakati wazo linapokujia katika ufahamu wako, iulize nafsi yako maswali matatu. Jambo hilo litampendeza Mungu? Litawasaidia watu wanaoteseka?
Kwa maneno mengine litakuwa msaada kwa watu? Litaleta mafanikio mazuri kwangu?
Kama jibu lako ni ndiyo katika maswali hayo yote matatu, utakuwa umekuwa na maono yenye mafanikio.
Unapoamua kufanya jambo fulani usijiulize ulize kuwa hii ni njia nyepesi ya mafanikio? Au ni njia rahisi?
Inaweza kuwa na usalama? Haitakuwa na vikwazo? Hakuna utakachoshindwa utakapofanya bidii. Hakuna mwenye nguvu ya kuua ndoto yako isipokuwa ni wewe mwenyewe.
Panga mipango. Huwezi kujenga jengo bila kuwa na ramani. Huwezi kufanikiwa matarajio yako pasipokuwa na malengo makubwa.
Ninamfahamu mtu mmoja aliyekuwa na maono makubwa lakini yalikuwa hayafiki mbali. Ni kwa sababu alikuwa hana ramani ya maono yake.
Hakikisha unatimiza ndoto uliyojiwekea. Malengo yako hayawezi kufanikiwa kama hujajitoa kufanya hivyo.
Ili kufanikiwa katika mipango yako kunahitaji juhudi na kufanya kazi kwa bidii. Ili upate mafanikio, endelea kufanya bidii.
Amua pa kuanzia. Fanya uamuzi. Panga muda wa kuanza. Usitafute sababu ya kuacha kuanza malengo yako kwa muda ulioupanga.
Katika dunia yetu kuna watu wengi ambao hupanga mipango mingi lakini hawaifanikishi. Jiondoe katika kundi hilo. Fanya kitu. Andika barua, piga simu. Anza hatua ya mafanikio.
Jiamini, waweza kutimiza ndoto zako. Wakati unajaribu kupata mafanikio utaona kuwa ni kipindi kigumu kwako.
Hali ya kukata tamaa inakuwepo katika moyo wako, ikisema jiondoe katika hatua ambayo unataka kuianza ya kupata mafanikio katika maisha yako.
Kama unakutana na kipindi cha majaribio katika biashara yako, ndoa yako, katika mambo yako binafsi, kwenye wingi wa watu, hali yako au hali ya maisha uliyoizoea na uko tayari kukabiliana nayo, songa mbele usikate tamaa.
Unachofanya ni kujaribu kupata mafanikio, tena mafanikio makubwa. Katika kila mafanikio unayoyapata, kuna gharama ya kulipa. Kumbuka huwezi  kupata ushindi bila kulipa gharama.

Jumamosi, 8 Agosti 2015

KIPAJI CHAKO NI UTAJIRI TOSHA KATIKA MAISHA YAKO

TAMBUA KIPAJI CHAKO.

                    ANAYEFANIKIWA     NI    YULE     ANAYEJIJUA ,   ANAYEJITAMBUA

MAFANIKIO   YA  PESA    kwa     asilimia  kubwa   yako  ndani   ya    KIPAJI  CHAKO.


Hapa    duniani ,  watu    waliofanikiwa   wana   kitu   kinachofanana.  WANAPENDA   WANACHOFANYA.  Huwezi   kuwakuta    watu     waliofanikiwa    WAKICHUKIA   WANACHOFANYA.   Tabia   hii   wanayo  watu   wanaojiona    ni   MASKINI.  Unafikiri  ni    MASKINI  WA   NINI ?     NI    MASKINI   WA  AKILI .  Tabia  yao    hawa     WANACHUKIA   WANACHOFANYA.


UNAWEZAJE    KUFAHAMU  KIPAJI  CHAKO ?

---Fikiria  MICHEZO  uliyokuwa  unapendelea    utotoni. Nini    ulikuwa   unapendelea  pindi    ulipokuwa  mdogo.  Ulifikiria   kuwa   nani   ukubwani  ?


---Waambie    rafiki   zako    wa    karibu    kuwa , unataka    KUTAFITI   KUJUA   KIPAJI     CHAKO    na    unahitajji   MAWAZO     YA   KWELI  KUTOKA  KWAO.


--TUNAJINYIMA    Wenyewe  FURSA   ya  kupata    PESA   kwa   sababu  ya    KUPUUZA   VIPAJI   VYETU.   Kila    MTU   ana   jambo  analoliweza ,  pia  kukiwa   na   MAMILIONI   YA     MAMBO  ASIYOYAWEZA

---TUWACHUNGUZE    WATOTO   WETU  WANAPENDELEA  NI NI  ?WANAWEZA  NINI  ?
---GUNDUA  KITU  UNACHOKIPENDA !! NA UANZE KUKIFANYIA KAZ MANA NDICHO KITAKACHO MTOA KIMAISHA.     

Innocent Massawe

HAKUNA MAFANIKIO BILA MALENGO ,amka sasa kazana

Funga macho, vuta picha ya magari mawili yanatembea. Dereva mmoja anajua kuwa anatoka kijiji A na kwenda kijiji B, halafu dereva wa pili wala hajui anakokwenda. Kati ya madereva hao wawili, yupi atafika anakokwenda?
Bila shaka jibu litakuwa ni dereva A. Kinachowatofautisha ni malengo, dereva wa gari la kwanza anajua kuwa lengo lake ni kufika kijiji B, hapo atatafuta hata njia ya mkato afike, hata kama hajui njia anaweza akauliza watu akaelekezwa. Dereva wa pili hata kama kuna barabara mbele yake anaweza akafika anakotakiwa kwenda, akapapita au akageuza maana hajui anakokwenda.
Hata kwenye maisha yetu hiyo ndiyo tofauti kubwa kati ya watu wenye malengo na wale wasiokuwa nayo. Wenye malengo huwa wanafanikiwa zaidi ya wale wasiokuwa nayo, yaani wanakwenda tu kama dereva wa pili!
Lengo?
Kuwa na malengo ni moja ya chachu kubwa ya mafanikio katika jambo lolote unalofanya kwenye maisha. Malengo yanakupa dira maishani mwako na kukuelekeza usiende mrama kwa kukosa mwelekeo.
Malengo yanaweza kuwa vitu vidogo tunavyotaka kubadili leo, pia yanaweza kuwa mambo makubwa tunayotaka kuyafanikisha siku zijazo, iwe baada ya mwezi, mwaka, au hata baada ya miaka mitano! Unaweza ukawa na malengo ya aina mbalimbali; ya kiafya, kikazi, kimasomo, kiuhusiano au kibiashara; muhimu ni kuwa na malengo.
Jiwekee malengo leo!
1. Fahamu unachokitaka
Ninachomaanisha hapa ni kujua nini unakitaka, ukijua unachokitaka utakuwa na msimamo wa kutaka kufikia malengo yako. Mwanafalsafa Lawrence J. Peter aliwahi kusema, ‘’If you don’t know where you are going, you will probably end up somewhere else.’’ Akimaanisha ... “Kama hujui unakokwenda inawezekana ukaishia sehemu nyingine tofauti kabisa.” Bado hujajua unachokitaka? Chukua kalamu na karatasi, kaa mkao wa kuandika! Jiulize, unataka kufanikiwa katika kitu gani? Hapa ni muhimu kuwaza ki- chanya chanya, usianze kudhani kwamba utafeli kabla hata haujajaribu. Jiamini. Kwenye karatasi yako sasa, orodhesha mambo yote unayotaka kufanikiwa, iweke mahali ambako utaiona mara kwa mara, wengine hutundika ukutani. Sasa anza kupanga mipango kwa kujiwekea malengo na kutekeleza moja baada ya jingine. Si lazima uanze na uliloandika kwanza.
2. Tambua nini kinakupa hamasa ya kutaka kufanikiwa
Motisha ni chachu ya ustahimilivu kwani hukufanya kuendelea kushikamana na mipango yako mpaka mwisho licha ya kuwa na vipingamizi vingi katika njia yako ya mafanikio. Malengo mengine ni ya muda mrefu hivyo yanakuhitaji uwe mvumilivu ili ufanikiwe, kama utakosa ustahimilivu unaweza kujikuta unakata tamaa mapema kabla ya kufi kia malengo. Motisha ni kitu pekee kinachokusaidia kukusukuma uendelee kutaka kufanikiwa hivyo ni heri kila malengo unayojiwekea yawe ni yenye kukupa kiu ya kutaka kufanikiwa kwa kuwa unapenda hayo unayoyahangaikia.
3. Jijengee nidhamu ya ufuatiliaji mpaka mwisho
Ndiyo. Wapo wenye tabia ya kushika hiki na kuacha, kisha kuanza kingine na kingine vyote vinaishia njiani. Kuwa na nidhamu, fi ka mwisho.
4. Tathmini hatua utakazopitia
Licha ya kutambua nini unataka, ni jambo la msingi kujua pia utasonga mbele. Wanasema safari ni hatua; Unaanzaje? Kuna vikwazo gani na utakabiliana navyo vipi? Inakufundisha nini? Pata picha halisi ya nini utafanya na wapi.
5. Amini inawezekana
Safari ya mafanikio siyo rahisi kama watu wengi wanavyofi kiria, kila aliyefanikiwa ana hadithi yake ya kusimulia juu ya changamoto alizokumbana nazo katika jitihada za kutafuta mafanikio. Kama hutokuwa na imani thabiti ya kile unachofanya ni vigumu kuwa na matumaini ya kufi kia mafanikio. Hofu na shaka vinaweza kukurudisha nyuma, usikubali, lakini usidharau, jipange.post na Innocent Priscus

BIASHARA NA MAFANIKIO

Tumekuwa tukisoma na hata kusikia mazungumzo ya kawaida na kwenye vyombo vya habari juu ya ndoto za wajasiriamali. Baadhi yao wamekuwa wakisema wanataka kuwa kama mfanyabiashara fulani maarufu kutokana na biashara wanazozifanya.
Haya ni mambo ya kawaida katika maisha kwani maisha ni wigo, lakini mwigo wenye uhalisia wa kweli kulingana na mazingira, wakati, uwezo na uthubutu wa mtu katika jambo analolifanya.
Katika kufanikisha yale ambayo unayafanya na hata unayotaka kuyafanya kwa mafanikio katika shughuli zako za ujasiriamali, huna budi kufanya mambo kadha wa kadha kama tabia zako za kila siku za utendaji wako wa kazi.
Jaribu kufikiria juu ya uwezo ulionao katika utendaji kazi wako kwani wajasiriamali waliofanikiwa wanajua udhaifu wao na hawathubutu kuona kama vitu vya kuwakwamisha katika shughuli zao, bali wanachukulia kama moja ya fursa za kufikia malengo yao.
Wajasiriamali waliofanikiwa hujaribu kutumia njia mpya kwa lengo la kuimarisha mbinu za biashara zao kwa kuhakikisha hawafanyi upotevu wowote wa rasilimali katika mchakato mzima wa uendelezaji na uendeshaji wa biashara zao.
Jaribu kufikiria juu ya wateja wako kwani wateja ndiyo roho ya biashara yako. Bila wao hakuna biashara, kwani hakuna familia yoyote hapa duniani ambayo imewahi kuendesha biashara kwa kujitegemea kama wateja wanaojitosheleza.
Jambo la msingi hapa ni kujua au kupata taarifa za jumla ya idadi ya watu, hususani wateja ambao watakuwa watumiaji wa bidhaa au huduma unazozitoa kwani ni muhimu kukumbuka kuwa mchakato wa kutafuta soko au kujaribu kuuza bidhaa kwa watu ambao hawahitaji bidhaa/huduma husika ni jambo la kupoteza muda na kujitafutia matatizo yasiyo ya msingi kama vile msongo wa mawazo na kukata tamaa ya maisha.
Wajasiriamali waliofanikiwa hujikita zaidi kutafuta masoko kwa watu wanaohitajika au wanaohitaji bidhaa husika, hivyo kutumia muda vizuri na rasilimali zilizopo.
Pindi wajasiriamali wa aina hii wanapogundua kuwa wanakidhi mahitaji ya wateja wao hutafuta njia au mbinu za kuhakikisha wanawakamata na kuwakumbatia wasiwaponyoke.
Wajasiriamali hawa hufanya kila juhudi ya kuanzisha uhusiano mzuri wa muda mrefu kwani tunaambiwa kuwa mjasiriamali mzuri ni yule anayeona bidhaa yake kupitia mahitaji au dhima ya mteja wake.
Kufikiria juu ya biashara yako ikiwa ni pamoja na kufikiria kile kinachoendela nje ya biashara yako hasa kile kinachohusu au kinachoshabihiana na biashara yako ili kuwa na uelewa mpana wa mambo mbalimbali yanayohusu shughuli unazozifanya.
Kufanya uchambuzi wa kina juu ya washindani wako wa biashara siyo tu kunakusaidia kujua unayeshindana naye bali pia kunakusaidia kujua matatizo au makosa yanajitokeza katika biashara yako ikiwa ni pamoja na tafsiri ya kina juu ya biashara yako kwa lengo la kuleta ufanisi katika utendaji kazi wako.
Ingawa si vizuri kufikiria makosa au kuanguka kwako kulikotokea siku za nyuma, ni vizuri pia ukatumia udhaifu au anguko la kipindi cha nyuma kama funzo la kuendesha mambo yako kwa mafanikio kwani wahenga wanasema binadamu hujifunza kutokana na makosa. Mjasiriamali wa kweli haogopi kushindwa, bali anafikiria zaidi namna ya kupata njia mbadala ya kurekebisha makosa yaliyotokana au yanayotokana na mchakato mzima wa shughuli za kijasiriamali kwa lengo la kupata mafanikio zaidi.
Mwandishi ni mtaalamu wa biashara