SIFA NA MIFANO YA MABANDA BORA YA KUFUGIA KUKU
Ujenzi wa mabanda bora ya kuku ni miongoni mwa mambo ya msingi kabisa katika ufugaji bora wa kuku wawe ni wa asili au wale walioboreshwa. Hata hivyo si kila mtindo wa ujenzi unafaa, kwahiyo ujenzi huo ni lazima uzingatie mahitaji halisi ili ufugaji huo uweze kutoa matokeo bora yanayotarajiwa na mfugaji.
MAMBO MUHIMU KATIKA UJEZI WA BANDA LA KUKU
1. Liingize hewa safi wakati wote.
2. Liwe kavu daima.
3. Liwe nafasi ya kutosha.
4. Liwe la gharama nafuu lakini la kudumu.
5. Lizuie kuingia wanyama na wadudu hatari kwa kuku.
6. Liwe na nafasi ya kuweka vyombo vya chakula na maji.
7. Lizuie upepo wakati wa baridi kali.